Na Farida Saidy Morogoro

Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA inatarajia  kufanya mashindano ya michezo maarufu kama Bandari Interpots Games ambayo yatajumuisha taasisi hiyo pamoja na taasisi nyingine ambazo zitashiriki mashindano hayo  yatakayofanyika Mkoani Morogoro kuanzia Septemba 13 hadi 20 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Afisa mawasiliano na mjumbe wa kamati ya michezo TPA Bwana Focus Mauki wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa ambapo amesema kutakuwa na michezo mbalimbali ambayo itafanyika katika uwanja wa jamhuri na kiwanja cha mpira wa wavu cha JKT Bwalo La Umwema vilivyopo mjini Morogoro.

Michezo itakayofanyika ni pamoja na mpira wa miguu, pete, wavu, kuvuta kamba kwa wanawake na wanaume pamoja na michezo mingine mingi, huku  mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano hiyo akitarajiwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Aidha amesema timu zitakazoshiriki ni pamoja na timu ya Bandari kutoka, Bandari ya  Dar  es Salaam,Tanga, Mtwara, Zanzibar  pamoja na timu  zinazoundwa na mikoa ya maziwa mkuu.
Ameongza kuwa kutokana na maombi mengi kutoka kwa  wadau wa michezo kutoka taasisi na sekta mbalimbali, mashindano ya mwaka huu yatashirikisha pia timu kutoka kitengo cha kontena kutoka bandari ya dar es salaam TPS, shirika la huduma za meli.

Hata hivyo amesema kuwa mamlaka ya bandari Tanzania TPA imetoa timu tano huku kukiwa na timu nyingine ambazo tayari zitashiriki kutokana na mashindano hayo kuwa na muamko mkubwa kila mwaka.

Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya maandalizi ya michezo TPA akiwemo mwenyekiti wa wafanyakazi kutoka Bandari ya Dar es salaam Mashaka  Karume na Priscilla Mkoka wamewataka wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa jamuhuri kushuhudia michezo mbalimbali.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...