*****************************
Zoezi la Uhakiki wa Uhai wa Vyama vya Siasa na Ufuatiliaji wa naamna vyama hivyo vinavyo tekeleza Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasasa (ORPP) lawa faraaja kwa Vyama vyote vyenye usajili wa Kudumu.


Msajili awapa kongole viongozi Vyama vya siasa,Aahidi kuendelea kuwa mlezi bora. Viongozi wa Vyama waimwagia sifa kedekede Ofisi y msajili kwa namna inavyo endesha zoezi la Uhakiki.

Zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siassa lilianza tangu tarehe 30 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam ambap mpaka sasa jumla ya Vyama 13 kati ya 19 vyenye usajili wa kudumu vikiwa vimekwisha hakikiwa huku yama sita ambavyo ni CCM, CUF, TLP, CHADEMA, UDP. ADA TADEA pamoja SAU vikiwa vimesalia kupitiwa na zoezi hilo linalotarajiwa kuhitimishwa mapema tarehe 28 Septemba jijini Dodoma.

Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni pamoja na Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 toleo la mwaka 2019 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi Sura ya 278 toleo la Mwaka 2015 pamoja na kanuni zake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...