Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli amefanya ziara kwenye eneo Bonyokwa Darajani kando kando mwa Mto Luhanga kwa lengo la kuangalia changamoto zilizopo ili kuzipatia ufumbuzi.
Katika ziara hiyo Mbunge Kamoli alikuwa ameongozana na Mhandisi wa Jiji la Dar es Salaam John Magori ambaye aliona eneo hilo ambalo kuna mwananchi kajitolea kufanya matengenezo hili kufanikisha barabara inayopita maeneo hayo inapitika wakati wote.
Mbunge huyo alilazimika kuwa na Mhandisi Magori baada ya kuwepo mtu mmoja anayetuhumiwa kutaka kukwamisha jitihada za mwekezaji huyo aliyejitolea kufanya matengenezo ya barabara.
"Nikiri suala hili ni la kitaalamu zaidi hivyo nimeamua kumuita Mhandisi wa Jiji la Dar es Salaam maana yeye ndio atatoa ushauri mzuri na wa kitaalamu,"amesema Mbunge huyo ambaye yupo kwenye ziara ya kutatua kwenye kero za wananchi katika jimbo lake.
Kwa upande wake Mwekezaji wa Hospital ya Harmony Memorial Polyclinic Jullyan Mmary aliyejitolea kufanya matengenezo hayo amesema lengo lake ni kuwasaidia wakazi wanaozunguka maeneo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli akiwa pamoja na Mhandisi wa Jiji la Dar es Salaam John Magori wakiangalia eneo ambalo mwekezaji kajitolea kurekebisha barabara.Picha zote na Shikunzi Oscar
Mbunge wa Segerea Bonnah Kamoli akipita Kandokando mwa Mto Luhanga eneo la Bonyokwa Darajani
Bonnah Kamoli akizungumza na wananchi wa Bonyokwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...