Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Meja Jenerali Gabriel Mhidze, ametoa mwelekeo wa bohari hiyo katika kutoa huduma nchini na kusema kuwa, ili kupunguza gharama za dawa na vifaa tiba, wameendelea na ujenzi wa viwanda na kuvifanyia maboresho vilivyopo.
Amesema tayari kuna viwanda saba vya MSD katika Mkoa wa Njombe na Dar es Salaam na baadhi ya viwanda hivyo vimeanza uzalishaji wa kutengeneza vidonge, vidonge vya rangi mbili, Sanitaiza,Barakoa , dawa ya majimaji na kutakuwa na kiwanda cha kutengeneza Cream ya kupaka
Akizungmza leo Septemba 28, 2021 jijini Dar es Salaam wakati semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na MSD kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali yakiwemo mafanikio na mwelekeo wa bohari hiyo Mhidze ameelezea kwa kina mikakati waliyonayo kuhakikisha watanzania wanapata huduma za afya kwa gharama nafuu zaidi.
"Wakati naingia hapa MSD Mei mwaka jana (2022), hali ilikuwa siyo nzuri, kwani tuliingia wakati wa janga la Covid - 19, barakoa ilikuwa ikiuzwa kwa bei ya juu, vitakasa mikoni navyo hali ilikuwa hivyo hivyo.
"Hata usambazaji wa dawa nao haukuwa mzuri, na sababu kubwa niliambiwa ni kutokana na Corona, nliwaita wataalamu tulionao hapa MSD na tukakusanya mawazo kupitia maandiko, kisha tukawawezesha (wataalamu) ili waanze kutekeleza," amesema.
Amefafanua kutokana na umuhimu wake, MSD ilianza kufanyia kazi andiko la kutengeneza barakoa, ili kuijengea nchi uwezo wa kuwa kifaa tiba hicho."Kabla ya hapo barakoa tulikuwa tunaagiza kutoka Afrika Kusini ambako nako zilikuwa zikiingizwa kutoka China.
"Tukaanza kutengeneza barakoa hapa nchini na kusaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto ya covid 19," alisema.
Mbali na barakoa, Meja Jenerali Mhidze, alisema baadae MSD iligeukia utengenezaji wa dawa, "tulianza na dawa moja na sasa tumefikia dawa 10."
KUHUSU MIPIRA YA MIKONO
Amesema MSD imeanzisha kiwanda cha kutengeneza mipira ya mikono kilichopo Idofya, Makambako mkoani Njombe."Tunatarajia Novemba tutakuwa na gloves (mipira ya mikono) yetu ya kwanza hapa Tanzania."
Kwa mujibu wa Meja Jenerali Mhidze, katika kipindi cha mwaka mmoja tangu alipoteuliwa kuongoza MSD, ameshirikana na wataalamu wa bohari hiyo kuongeza kasi ya uzalishaji dawa na vifaa tiba kwa kufufua na kuvipa uwezo wa kuzalisha viwanda vilivyopo.
"Hapa Keko MSD tuna kiwanda cha 'Creem' na mafuta yanayotumiwa na watu wenye ulemavu wa ngozi, pia tutakuwa na kiwanda cha dawa ya kusugulia meno," alisema.
UTOAJI HUDUMA HOSPITALI
Amesema kuwa awali eneo hilo lilikuwa likiigharimu fedha nyingi za Serikali, kutokana na gharama kubwa za uagizaji au ununuaji wa mashine za kupimia maradhi na nyingine muhimu katika utoaji huduma za afya kwa wananchi.
Hivyo amesema kwa kuona changamoto gharama hizo MSD ili kwenda kuzungumza na watengenezaji wa vifaatiba hususan mashine muhimu zinazohitajika kwa wingi katika utoaji huduma.
Meja Jenerali Mhidze amesema lengo la kuzungumza na watengenezaji ni kuiwezesha MSD kununua mashine nyingi kwa gharama nafuu, ili nayo izitoe mashine hizo kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya katika maeneo mbalimbali na hatimae kumwondolea mwananchi ulazima wa kutembea umbali mrefu kufuata baadhi ya huma.
Pia amesema kwa kutambua umuhimu wa huduma ya uchujaji damu, wameamua Kuleta mashine za kuchuja damu kwa gharama nafuu ili wananchi wapate huduma kwa gharama nafuu.
"Tutakwenda na kasi ya Serikali katika ujenzi wa vituo vya afya kwa sisi kuufikisha mashine hizo ili ziendelee kutoa huduma.Tumeona upo umuhimu wa kushirikiana na wafanyabiashara ili kuongeza fursa ya utoaji huduma bora kwa wananchi na mipango tuliyonayo haina nia ya kuua biashara ya wafanyabiashara,"amesema.
.
Akizungumzia kwa kifupi muelekeo wa MSD baada ya kuelezea mafanikio waliyoyapata ,Meja Jenerali Mhidze amesema muelekeo ni mzuri na yajayo yanafurahisha na matamanio yake ni kuona nchini Tanzania kunakuwa na viwanda vingi vya kutengeneza dawa na vifaa tiba.
Meja Jenerali Gabriel Mhidze ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD (kulia) akiwa amekaa kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
Waandishi wa habari wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika leo Septemba 28,2021 jijini Dar es Salaam
Baadhi ya maofisa wa MSD wakiwa kwenye semina hiyo
Maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa(MSD) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakijitambulisha kwa waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa semina iliyoandaliwa na MSD
Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki kwenye Semina iliyoandaliwa na MSD wakiwa makini kumsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Mhidze.
Sehemu ya maofisa wa Bohari Kuu ( MSD) wakiwa makini kumsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Mhidze ( hayupo pichani)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...