NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO.
MTANDAO wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) tawi la Namtumbo wamepata viongozi wapya wa tawi watakaoongoza tawi hilo la MVIWATA wilaya ya Namtumbo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu ijayo .

Akisoma matokeo baada ya uchaguzi huo katibu tawala wa wialaya ya Namtumbo bwana Aden Nchimbi alitaja majina ya wajumbe waliochaguliwa katika mkutano huo kuwa ni Magnus Ndunguru,Issa Omari ,Fatuma Ngonyani ,Juma Tweve ,Mariamu Mchopa ,Lusiana Komba na mwingine ni Amiri Komba.

Kwa mujibu wa katiba ya MVIWATA wajumbe hao waliochaguliwa katika mkutano huo waliketi na kuchaguana katika nafasi mbalimbali kuanzia nafasi ya mwenyekiti,makamu mwenyekiti,mwekahazina ,katibu na wengine kubaki wajumbe .

Baada ya wajumbe kuchaguana katika nafasi hizo nafasi ya mwenyekiti ilichukuliwa na Magnus Ndunguru ,Lusiana Komba makamu Mwenyekiti ,Juma Tweve katibu huku nafasi ya Mwekahazina ikichukuliwa na Issa Omari.

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Ningu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika katika mkutano huo aliwataka wanachama wa MVIWATA kuchagua viongozi wanaoweza kujitoa katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ,kuchagua viongozi watakaowajali wakulima walio na uadilifu na uaminifu.

Pia Dkt Ningu aliwataka wanachama kuacha kuchagua viongozi kwa kufuata ushabiki,ujirani ,kufahamiana bali wachague viongozi wenye uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kuwaunganisha ,kuwashirikisha na kuwaleta wakulima pamoja ili kuleta matokeo chanya yanayolengwa na MVIWATA kwa wakulima wadogo wadogo wa wilaya Namtumbo.

Hata hivyo Dkt Ningu aliwahakikishia viongozi waliochaguliwa kuwapa ushirikiano wa kutosha ili wafanye kazi zao za kuelimisha wakulima kujiunga na MVIWATA katika wilaya ya Namtumbo na akaahidi pia kufuatilia shughuli za wanachama wa MVIWATA katika wilaya hiyo ili kupima matokeo ya MVIWATA kwa wanachama wake wilayani humo alisemaDkt Ningu,

Mwenyekiti wa MVIWATA mkoa wa Ruvuma alimhakikishia mkuu wa wilaya ya Namtumbo kuwa maagizo na ushauri uliotolewa utazingatiwa hasa wa kuongeza wanachama pamoja na upimaji wa matokeo yanayofanywa na MVIWATA kwa wanachama wa wilaya ya Namtumbo.

Naye Laika Haji Mratibu wa MVIWATA mkoa wa Ruvuma alisema vikundi 7kutoka katika kata saba ya Ligera,Hanga,Kitanda,Mkongo,Rwinga,Limamu pamoja na kikundi kutoka kata ya Luchili ndio wanachama wa MVIWATA wilaya ya Namtumbo kati ya kata 21 za wilaya hiyo.

Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) ilianzishwa na wakulima wenyewe mwaka 1993 na kauli mbiu ya MVIWATA ni sauti ya wakulima na mtetezi wa wakulima ni mkulima mwenyewe .

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Ningu akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa MVIWATA wilaya ya Namtumbo na picha ya pili viongozi wapya wa MVIWATA wilaya ya Namtumbo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...