Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari akimwongoza Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara mara baada ya kuwasili makao makuu ya mamlaka hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea mamlaka hiyo ili kujionea utendaji wa mamlaka hiyo.
Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara(kulia) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuona ufanisi unaofanywa na mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza S. Johari.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari akitoa maelezo kuhusu kazi na miundo mbalimbali ya Mamlaka wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara alipotembelea mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akizungumza na viogozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) mara baada ya kupata maelezo kuhusu utendaji wa Mamlaka hiyo leo alipotembelea Mamlaka hiyo. kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) wakimsikiliza Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara alipokuwa akitoa maelekezo kuhusu utendaji kazi wa mamlaka hiyo wakati wa ziara yake kwenye Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga, Aristid Joseph Kanje akitoa ufafanuzi kuhusu kozi zitolewazo na chuo hicho mara baada ya Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara kutembelea Mamlaka hiyo pamoja na Chuo hicho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari
Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi Chuo cha Usafiri wa anga, Neema Aberd Senyagwa kuhusu namna wanafunzi wanavyojifunza mfumo wa kuongoza ndege wakati wa ziara yake kwenye Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) leo Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara mara baada ya kupewa maelezo ya ujenzi wa chuo cha kisasa cha usafiri wa Anga katika eneo la kiwanja cha Mamlaka hiyo.
Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) mara baada ya kutembelea kiwanja kilichotengwa kwa ajili ya ujezi wa chuo cha kisasa cha Usafiri wa Anga
Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) pamoja na wafanayakazi wa TCAA walikuwa kwenye mafunzo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Terminal 1 alipowatembelea ili kuona mafunzo yanayotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) pamoja na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...