Na.Mwandishi wetu, Michuzi Tv
KAMPUNI ya Creative Consultancy Zanzibar pamoja na Mamlaka ya Udhibiti huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) wametangaza rasmi Mbio za Upendo Nakupenda Marathon, mbio zenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya taulo za kike kwa wasichana wa shule za sekondari na wenye uhitaji, pamoja na kutoa elimu kwa wasichana.
Mbio hizi zinafanywa kwa ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Chama cha Riadha Zanzibar.
Mbio zitakuwa na Kilimotia 1(miaka 7-13) kwa watoto na wenye ulemavu, Kilometa 5 kwa ajili ya wote, 10km na 21km.
Mbio zimepangwa kufanyika Oktoba 16 mwaka 2021 na shughuli zitaanza Oktoba 14 kwa Usafi, na Oktoba 15 shughuli ya Wizara ya Afya kuadhimisha siku ya unawaji mikono duniani.
Mbio hizi gharama yake ni Shilingi 25,000 kwa wote na 5000 kwa watoto na wenye ulemavu.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Mafunzo ya Amali Khamis Ali akiwa kwenye picha ya pamoja na Waandishi Wahabari pamoja na Muwakilishi kutoka kamati ya Maandalizi "Nakupenda Marathon" Benedict Anthony Mara baada ya kuzindua rasmi mbio yenye kulenga kusaidia taulo za kike Mashuleni Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...