Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
SHIRIKA la bima la Zanzibar (ZIC) wadhamiria kujitolea Kudhamini Tamasha la wajasiriamali wanawake Mkoani Mtwara linalotarajiwa kufanyika mapema septemba 19 mwaka huu Mkoani Mtwara.
Akizungumza na Michuzi Tv , Mkurugenzi wa shirika hilo Arafat Haji Mara baada ya kukutana na Mkuu wa wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya nakuzungumza mengi amesema kwa mara nyingi shirika hilo limekua likitoa huduma katika Mkoa huo hivyo ni wakati wa kurejesha kwa wateja wao.
"Tulikua tunatoa huduma zetu hapa Mtwara hivyo tuna njia nyingi za kurejesha kwa jamii hususani wateja wetu na hata wasio wateja wetu na tumehaidi kuwepo katika Tamasha la wajasiriamali wanawake ambapo kimsimgi kuwaunga Mkono wanawake hao."
Hata hivyo Haji ameeleza kuwa katika Tamasha Hilo wataweza kutoa Elimu kwa wanawake hao wajasiriamali kwa namna gani wataweza kujilinda na kutumia bima kwa maslahi ya familia zao pamoja na Biashara zao kwa ujumla.
Mkurugenzi wa wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya pichani akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la bima Zanzibar (ZIC) Arafat Haji pamoja na wawakilishi wengine kutoka Shirika Hilo Mara baada ya kukutana na kujadili Tamasha la wanawake wajasiriamali mkoani Mtwara ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 19 mwaka huu Mkoani Mtwara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...