KUANZISHWA kwa safari za mabasi ya mwendokasi kutoka kutoka Morocco kwenda Kawe, kumepokelewa kwa namna tofauti na wananchi amao hasa ndio watumiaji wa usafiri huo pamoja na madereva wa daladala.
Abiria wamelipokea vizuri hili swala, kwani linawasaidia kuepukana na msongamano wa kwenye daladala huku madereva wakiona kama ni msalaba kwao kwani mafuta yamepanda bei na abiria inawapasa kunyang'anyana kwa sasa.

Hayo yamezungumzwa na wananchi wa jiji la Dar es Salaam leo Agosti 6,2021 kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na Michuzi Tv, wamesema kuwa kwa sasa wananchi tonauwezo wa kuchagua ni usafiri upi tutumie pale tunapotaka kufika Kawe au Mwenge.
Abdukarim Ibrahim amesema kuwa kuwepo kwa magari ya Mwendokasi katika barabara ya magari yanayoenda kawe kutokea morocco yatapungumza msongamano katika magari.
"Kwa mwendokasi kupitia huku Morocco kuelekea Kawe na Mwenge kwangu nachukulia ni swala zuri, kwasababu mara nyingi magari yanakuwa yanajaa halafu ukizingatia tupo kwenye wimbi la tatu la CORONA."Amesema Abdukarim Ibrahim (abiria).
Lakini pia madereva wamekuwa na maelezo yao kuhusiana na hii safari mpya iliyoanza ya mwendokasi.
"Mi nachukulia poa tu, kwasababu hii ni njia pia ya kujipatia riziki.Hamna anaependa kukaa na njaa, sote tunatafuta hela."Amesema dereva Rashid.
"Kwa upande wangu sijapenda, kwasababu huku ni kuzibiana riziki kwanini wasingepelekewa watu wa kivukoni kwasababu huku hamna shida ya magari."Ameongezea dereva Ismail.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...