JAJI wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu "Mahakama ya Mafisadi", Elinaza Luvanda amejitoa kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Hatua hiyo imekuja leo Septemba 6, 2021 baada ya Mbowe kumuomba Jaji Luvanda ajitoe katika kesi hiyo kwa madai ya Kkuwa hana Imani nae na kwamba hawatatendewa haki Katika shauri hilo.

Katika Maelezo Yake Mbowe akielezea kwa nini hana imani ni Jaji Luvanda amedai, ametoa madai Mbalimbali katika shauri hilo ikiwa ni pamoja na kutupilia mbali kila mapingamizi yanayowasilishwa na Upande wa Utetezi.

Pia amedai, Mapingamizi yanayowasilishwa na upande wa utetezi hayazingatiwi na kwamba hata vifungu vya sheria wanavyotumia kama mfano kwenye kuteteza mapingamjzi yao havizingatiwi wakati wa kutoa uamuzi wake jambo ambalo anadaia ni ukiukwaji wa haki za msingi.

Hata Hivyo mbowe amendelea kudai kuwa kesi hiyo ina hisia kwa jamii ni hivyo ni vyema hatua zote za usikilizwaji wa kesi hiyo uwe wazi bila uonevu.

Mbowe amedai ni ukweli Usio Pingika kuwa hisia za Jamii katika kesi hiyo zinadhibitishwa na mijadala mbalimbali inayoendelea katika mitandao ya kijamii ambayo ameisoma mbele ya mahakama Hiyo.

Mbowe amedai katika mitandao hiyo inasomeka kuwa Jaji Luvanda ni mtu wa TISS na waserikali na amewekwa katika mahakama ya Mafisadi kimkakati kwa lengo la Kumfunga Mbowe.

Kufuatia hilo Mbowe amemuomba Jaji Luvanda ajitoe katika kesi hiyo Ili atunze heshima yake na ya mahakama ili kuepuka lawama ambazo hastahili kuzipata.

Baada ya Mbowe Kuhitimisha madai yake, wakili wa Jamhuri Robert Kihando akapinga maombi yaliyowasilishwa na Mbowe akidai kuwa katika kesi hiyo hakuna mazingira yanayoruhusu Jaji Kujiondoa katika shauri hio.

Hata Hivyo upande wa Utetezi Ukiongozwa na Wakili Peter Kibata umedai kuwa hauna pingamizi dhidi ya Maombi y hayo ya Mbowe ambaye ni mshitakiwa wa nne katika shauri hilo

Baada ya pande kusikilza hoja za pande zote Jaji Luvanda akafikia uamuzi huo wa Kujitoa katika Kusikiliza Kesi hiyo kama ambavyo mshtakiwa ameomba akisema kuwa hakuna sababu za kujitetea kwenye hoja ambazo hazina msingi badala yake ni kujiondoa tu.

Kufuatia uamuzi wake huo wa kujiondoa Jaji Luvanda ameahirisha kesi hiyo hadi pale itakapopangiwa Jaji mwingine.

Mapema leo, kesi hiyo iliitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa uamuzi wa mapingamizi matatu yaliyowasilishwa na upande wa utetezi.

Katika mapingamizi hayo mawili kati ya hayo yametupiliwa mbali huku moja la makosa kujirudia rudia kwenye hati ya mashtaka likukubaliwa.

Kufuatiwa kukubaliwa kwa hilo moja Jaji akautaka upande wa Jamhuri kufanya marekebisho katika hati ya mashtaka Ili kuondoa kasoro zilizopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...