Na Khadija Seif, Michuzi Tv
PETIT Money amewaomba Mashabiki wa King'amuzi cha Startimes kulipia Mapema ili kushuhudia shughuli ya Mtoto wake Kian mapema septemba 11 mwaka huu.
Akizungumza na Michuzi Tv, Petit Money amesema kupitia ubalozi wake na Kampuni ya Startimes wameipa nafasi ya shughuli kuonyeshwa kupitia chaneli ya Tv3 ili kuwapa nafasi Mashabiki zake kushuhudia uondo huo wa aina yake.
Hata hivyo Petit Money ameweka wazi kuwa Mzazi mwenzie (Esma platinum) alimtafuta baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na kutaka warudiane lakini kupitia shughuli hiyo ataweka wazi na kuvunja ukimya wake.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa ameeleza kwa namna Mashabiki hao wanaweza kushiriki tukio Hilo kubwa alilolipa jina la "Nalimwaga".
"Wanachotakiwa ni kulipia ving'amuzi vyao Ili waweze kuona tukio Hilo kubwa la aina yake ambalo litawapa nafasi ya Mashabiki wa mitandaoni nao waweze kuliona bila chenga kupitia tv3". Amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...