Charles James, Michuzi TV

KUFUATIA kupewa wito wa kufika kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Wabunge Jerry Silaa wa Jimbo la Ukonga na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Humphrey Polepole wamewasili na kuhojiwa kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dodoma.

Wito huo kwa Wabunge hao ulitolewa na Katibu wa Wabunge wa CCM, Rashid Shangazi ikiwa ni kutii maagizo ya Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyoyatoa kufuatia kukutwa na makosa mbalimbali na Kamati ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge kwa Wabunge Jerry Silaa na Josephat Gwajima wa Jimbo la Kawe.

"Kama ambavyo juzi Mhe Spika Ndugai alivyokua akihitimisha azimio la Bunge kuhusu Kamati ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge alitoa maagizo ya kuhojiwa kwa Wabunge Silaa na Gwajima kwenye Mamlaka zingine, hivyo sisi Chama Cha Mapinduzi kwenye mhimili wa Bunge tumeona ni vema kuwaita wanachama wetu hawa ili tuweze kuwahoji kwenye kamati ya Maadili ya Wabunge wa CCM kuhusu masuala tofauti," Alisema Shangazi.

Kufuaia agizo hilo leo asubuhi Mbunge Silaa na Polepole kwa nyakati tofauti wamefika kuhojiwa na Kamati hiyo ya Maadili ya Wabunge wa CCM.

" Kikao Cha Maadili ni kikao cha ndani, kwahiyo taarifa zote zitatoka kwa utaratibu wa Chama, Asanteni sana," Amesema Polepole wakati akizungumza na wandishi wa habari baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati hiyo Makao Makuu ya CCM Dodoma.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...