Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 06 Septemba, 2021 amewasili katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara akiwa na kundi la wapiga picha wa kipindi cha Royal Tour kwa ajili ya kuendelea kuonesha na kuelezea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kupitia filamu itakayoandaliwa na timu hiyo.
Mhe. Rais Samia amewaambiwa wananchi wa Wilaya hiyo waliojitokeza kumpokea kuwa filamu hiyo itakapokamilika itatangaza maeneo yote yenye vivutio vya utalii nchini na kuchochea uchumi wa nchi kupitia watalii, wawekezaji na wafanyabiashara.
Aidha, Mhe. Rais amesema filamu hiyo pia itaelezea hali halisi ya siasa zilivyo nchini tofauti na baadhi ya mataifa mengine inavyoelezea.
Amesema kwa sasa wahisani wengi wametoka katika utoaji wa misaada na kujikita katika biashara, hivyo filamu hiyo itasaidia kueleza na kuonesha maeneo mbalimbali ya utalii ambayo yatatoa furza za biashara na uwekezaji.
Pia, Mhe. Rais Samia amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Serengeti kuwa ahadi zote zilizotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 zitatekelezwa.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Serengeti Mkoani Mara leo Sept 06,2021 kwa ajili kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini. PICHA NA IKULU.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...