Na Humphrey Shao, Michuzi TV

MKUU Wa Mkoa Dar es Salaam Amos Makalla amekerwa na mchakato wa umaliziaji wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti na kusema kuwa hajaridhishwa na utendaji kazi wa machinjio hayo mapya ya kisasa.

Makalla alisema kuwa leo ni mara ya pili anafika Vingunguti kutemblea mradi huo.

"Mradi huu ulikuwa kwenye bajeti ya awamu ya tano nakuendelea Awamu ya Sita kwa matarajio ya kuchinja ng'ombe 1000, mbuzi 1000 na kondoo 500 kwa siku,  kwa ajili ya soko la ndani na kusafirisha nchi zingine haswa Oman na Dubai Machinjio hayo hayajaanza kufanyakazi kwa sababu ya kukosa  chumba cha baridi cha kuhifadhi nyama,hivyo haiwezi kutumika," alisema Makalla.

Makalla alisema ameiomba l kwa Waziri wa Mifugo kusimamia mradi huo mpaka utakapo anza kutumika.

Ametaja kuwa matarajio ni kukuta  machanjio hiyo imeanza kufanya kazi na kuchinja ng'ombe, mbuzi na kondoo ila kilichokamilishwa ni majengo tu na kushangaa kuona bado machinjio hayana uwezo kwani yamekosa sifa kutokana na kutokuwepo kwa chumba cha baridi.

“Nilipokuja nilikuwa nafatilia ahadi ya waziri Mkuu uliotolea na watendaji kazi wa machinjio hii ambapo alitarajia kufika Julai mosi utakuwa umekamilika , na mim nilipo kuja mliniahidi kuwa kufikaJulai  27 utakuwa umekamilika kwa sasa naona hali ni ileile"  alisema Makalla.

 Hata hivyo RC Makalla amemwelekeza Kaimu Mkurungezi wa Jiji la Ilala, Tabu  Shaibu na timu ya manunuzi kukaa kikao na kutafuta mkandarasi kukamilisha ununuzi wa  vifaa vinavyo itajika ili chumba cha baridi kikamilke ili machinjio hiyo ianze kufanya kazi kama yalivyo matarajio ya wananchi.

Naye, Tabu Shaibu amemwahidi Makala ifikapo Septemba 13 watakuwa wamepata mkandarasi ili kuendelea na mikakati mingine ya ununuzi wa vifaa hivyo na kukamilisha chumba cha baridi.

Makala aliwaambia baada ya hapo waelekee kwa katibu  tawala vifaa hivyo vitasafirishwa kwa msaada wa mkoa kwa kuwa hakuna tatizo la kifedha na kuomba taarifa ya kila siku kuhusu mradi huu.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...