Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

MCHEZO wa marudiano kati ya Waandishi wa Habari za Michezo Waliooa na Wasiooa FC utapigwa Jumamosi ya Septemba 18, 2021 katika uwanja wa TTC Chang’ombe (Gwambina Lounge), Wilayani Temeke Dar es Salaam ikiwa lengo kubwa kuwaweka pamoja Wanahanari hao kupitia tasnia ya Michezo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam, Mratibu wa mchezo huo, Mwanaidi Suleiman amesema lengo kubwa ni kuwaweka pamoja Wanahabari sambamba na kubadilishana uzoefu kati ya wazoefu na wale wanaotoka vyuoni na walioingia kwenye tasnia hiyo hivi karibuni.

Mwanaidi amesema mchezo wa mwaka jana ulichezwa Wilayani Ubungo, Dar es Salaam walikuwa na lengo la kuhamasisha kujikinga na kutoa elimu kuhusu janga la virusi vya Uviko-19, ambao ulikuwa tishio kwa Watanzania na duniani kwa ujumla, amesema mchezo wa msimu huu utaenda sambamba na elimu ya kupata Chanjo dhidi ya Uviko-19.

“Kabla ya mchezo huo Waandishi wa Habari watapata semina kuhusu Rushwa kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mahsusi kutoa elimu ya Rushwa Michezoni na kuhamasisha Jamii kuepuka Rushwa katika nyanja mbalimbali”, amesema Mwanaidi.

Kwa upande wa Nahodha wa Waliooa FC, Anwari Binde ameahidi kupata ushindi katika mchezo huo baada ya Wachezaji wengi wa Wasiooa FC kupindi kile, sasa kupata Ndoa na kuhamia kwa Waliooa FC akitoa Mfano kwa Mchezaji Abdul Mkeyenge ambaye amepata Jiko hivi karibuni. Pia Binde amewashauri Wasioa kuoa na kuondokana na ubachela.

Mchezaji wa Waliooa FC, Alwatan Ramadhan Ngoda kwa niaba ya timu yao wameahidi kulipa kisasi katika mchezo huo, baada ya mchezo wa msimu uliopita kupoteza kwa mikwaju ya Penalti. “Tutawafunga vizazi na vizazi havitasahau kwa kipigo tutakachowapa siku huyo pale TTC Chang’ombe”, amesema Ngoda.

Mchezaji wa Wasiooa FC, Mbwiga Mbwiguke amesema wataendeleza ushindi katika mtanange huo, kutokana na kuishi kwa wasiwasi Wachezaji wa timu ya Waliooa FC majumbani kwao.

Kuelekea mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la TCC Chang’ombe, Wadhamini K4S Security wametoa vifaa vya mchezo huo zikiwemo Jezi maalum, Mipira sambamba na kuahidi Ulinzi wa kutosha wakati wote wa pambano hilo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...