Na. Rahma Taratibu, Sandra Charles na Regina Frank, SJMC, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (Mb), ameeleza kuwa Serikali inaangalia njia bora itakayosaidia kuboresha utaratibu wa maombi na vigezo vya uandaaji wa miradi ya kimkakati kabla ya utoaji wa fedha.
Mhandisi Masauni alisema hayo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Manyoni Mashariki Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuhuisha vigezo vya mfumo wa Miradi ya Kimkakati kupitia maandiko ya miradi ili iweze kusaidia Halmashauri kubuni miradi ya kiuchumi.
“Fedha za kugharamia miradi mkakati hutolewa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na Wizara ya Fedha na Mipango hivyo, hoja ya Mbunge kuhusu uboreshaji wa vigezo vilivyowekwa kwenye uchambuzi wa miradi ya kimkakati imechukuliwa,” alisema Mhandisi Masauni.
Aidha, Mhandisi Masauni alieleza kuwa, Serikali imejikita katika kutoa huduma bora na zenye uhakika kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaendelea kujiongezea mapato kwa kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao.
“Ili kufikia lengo hili Serikali iliandaa mkakati maalum wa kuziwezesha Halmashauri kujitegemea kimapato kwa lengo la kupunguza utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali kuu”, alieleza Mhandisi Masauni.
Aliongezea kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatakiwa kuhakikisha zinatumia kwa ukamilifu fursa za kimapato zilizopo katika maeneo yao na kuongeza uwezo wa kujitegemea kimapato.
Naye Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Kirumbe Ng'enda (Mb), alihoji hatua ya Serikali katika kujenga uwezo wa halmashauri sambamba na kuinua hali za wananchi kwa kupunguza riba za benki nchini ili waweze kushiriki vizuri katika miradi ya kimkakati katika halmashauri zao.
Akijibu swali hilo Mhandisi Masauni alisema kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa Serikali kuangalia jinsi ya kupunguza riba ambapo katika maeneo matano ambayo Benki Kuu ya Tanzania ilianisha kama njia ya kuweza kufikia malengo hayo tayari yameanza kufanyiwa kazi.
“Benki kadhaa tayari zimeanza kuwasilisha maombi Benki Kuu ya Tanzania ili kuweza kutumia fursa hizo zilizotolewa zenye dhamira ya kufikia malengo hayo kuhakikisha kwamba riba inakuwa nafuu kwa kiwango kisichozidi asilimia 10,” alisema Mhandisi Masauni.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kilolo Mhe. Justine Lazaro Nyamoga (Mb), a
Akijibu swali hilo Mhandisi Masauni alisema kuwa dhamira ya Serikali katika miradi ya kimkakati ni kuona inakuwa na tija na kuweza kujiendesha kwa faida hivyo hati chafu inapokuja inatoa kiashiria hasi cha ufanisi wa mradi husika.
Aliongeza kuwa jambo hilo litawasilishwa kwa wataalamu ili kuona namna ya kulifanyia kazi bila kuathiri lengo halisi la kuona tija inapatikana katika mradi husika lakini lisiathiri wananchi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) akijibu swali bungeni, jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...