UJAUZITO WA VANESSA MDEE WAMUIBUA JUX...ASHINDWA KUVUMILIA, AMTUMIA UJUMBE
Na Jamaly Mussa, DSJ
MSANII wa muziki wa kizazi kipya maarufu Bongo Fleva Juma Jux ameamua kumtumia ujumbe kwa aliyekuwa mpenzi wake wa zaamani Vanessa Mdee kwa kukwambia hana Neno na anamtakia kila la heri katika maisha yake ya sasa.
Jux ametuma ujumbe huo ikiwa ni siku chache tu Vanessa kuweka picha inayomuonesha akiwa na ujauzito wa mpenzi wake Rotimi wanayeishi naye nchini Marekani.Vanessa ana ujauzito wa miezi sita.
Vanessa moja ya Siprise aliyoifanya ni kuficha ujauzito huo kwa muda wote hadi alipoamua kuonesha picha akiwa mjamzito kupitia ukurasa wake wa Instagramu
Baada ya Venessa kuweka picha hiyo huku akiwa na mpenzi wake,Jux ameshindwa kuvumilia ,hivyo ametuma ujumbe kwa mwanadada huyo kupitia wimbo wake mpya ambao ameupa jina la Hana Noma.
Iko hivi, huko mitandaoni kumekuwepo na mjadala mkubwa na mmoja wa mashabiki wa Vanessa Mdee aliamua kumshambulia Jux,hivyo akaona badala ya kukaa kimya ni bora akatoa ya moyoni kupitia wimbo huo.
Katika wimbo huo sehemu ya mashairi yanasema hivi; "Awe na furaha na amani hamchukii bali anamuombea maisha yenye furaha." Ujumbe huo ni maalum kwa Vanessa Mdee ambaye walikuwa na mahusiano kwa muda mrefu lakini hawakubahatika kupata mtoto
Jux ndani ya kibao hicho hakusita kueleza jinsi ambavyo hana chuki yoyote na Vanessa, na kwamba maisha lazima yaendelee na yaliyopita huko nyuma yameshapita na sasa ni wakati wa kila mmoja kufurahia maisha anayoishi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...