Sekta ya usafirishaji imekuwa kwa haraka katika nchi nyingi barani Afrika kutokana na kuwepo kwa usafiri wa kukodi ambako wateja wanatafuta kupata usafiri salama na wenye gharama nafuu.  Kanda ya Afrika Mashariki vile vile unashuhudia kukua kwa usafiri wa kukodi ambapo huduma mbalimbali kama vile Bolt wanatoa huduma kupitia katika mfumo wao uliyopo katika application ya simu.

Soko la kukodi usafiri kwa njia ya mtandao (E-hailing Market) katika Afrika na Mashariki ya Kati lilitazamiwa kukua kufikia Dola bilioni 7.3 kufikia mwaka 2023. Sababu kubwa zinazochochea kuwepo kwa mahitaji ya usafiri wa kukodi katika kanda hii ni pamoja na kukua kwa miji, ongezeko la idadi ya vijana, kuongezeka kwa uwekezaji unaofanywa na watoa huduma za usafiri wa kukodi na ongezeko la idadi ya watumiaji wa simu za janja (smartphone) na mtandao wa internet.  

Tanzania haiko tofauti na nchi nyingine, kutokana na ongezeko la watumiaji wa mtandao wa internet na smartphone, watu katika miji na majiji kama vile Dar es salaam, Dodoma, Mwanza na Arusha wanapata fursa ya kufurahia huduma ya usafiri wa kukodi ambayo imeleta mabadiliko makubwa katika namna ambavyo watu wa mijini wanavyosafiri.

Akitoa maoni kuhusu maendeleo ya huduma ya usafiri wa kukodi katika soko la ndani, Maneja wa Bolt Tanzania, Remmy Eseka amesema kwamba huduma ya usafiri wa kukodi unashuhudia ukuaji mzuri.

"Mfumo wa usafiri wa kukodi kuendana na mahitaji wa Bolt unatoa njia rahisi na salama ya uombaji wa usafiri pale unapohitajika jambo ambalo linalowezesha watumiaji kujipatia usafiri kama wanavyohitaji na kwa gharama nafuu.   Huduma zetu zinahakikisha kwamba wateja wanaweza kufahamu kwa usahihi ni wapi gari lilipo, wanaweza kufuatilia safari zao na wanaweza kuchukuliwa na kushushwa mahali popote wanapohitaji, jambo linalopelekea huduma zetu kuongezeka umaarufu," Remmy Eseka, Maneja wa Bolt amebainisha mambo haya kuwa ndio sababu kuu ya ukuaji imara wa kampuni yake. 

Kwa kuongezea, urahisi wa kuagiza usafiri na faraja anayopata abiria kutokana na huduma ya kukodi usafiri kulingana na mahitaji unaweza kuchochea ukuaji zaidi katika tasnia ya usafiri wa kukodi Afrika hapo baadae.

"Bolt vile vile inachangia katika kukua kwa "Uchumi wa madereva" ambapo tunatoa mfumo wa Bolt kama chanzo kikuu na wakati mwingine kama chanzo cha ziada cha kiuchumi kwa madereva ambao wanataka kutekeleza majukumu mengine na wakati huo huo wakiwa wanaweza kuhudumia maisha yao.

 Mfumo huu umewasaidia madereva kuwa na uwezo kamili wa kuutawala muda wao na kiwango cha fedha ambacho wanaweza kujipatia,  Alihitimisha Eseka.

Mwaka 2017, shirika la Global Sachs lilitabiri kuwa miaka 10 ijayo itakuwa na mabadiliko makubwa zaidi katika jinsi ambavyo watu na bidhaa wanavyosafiri kuliko ilivyokuwa katika miongo mingine tangu kuvumbuliwa kwa vyombo vya usafirishaji.

Kadri ambavyo dunia inajitahidi kukabiliana na kujifunza kuishi na janga la Covid-19, teknolojia mpya zinazochipukia na mifumo ya biashara kama usafiri wa kukodi, magari yanayojiendesha yenyewe na huduma ya usafririshaji wa mizigo, vyombo vya usafiri vya kukodi na hata eVTOL (magari yanayoruka) yanachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha faida katika huduma ya usafirishaji ambayo kituo cha utafiti cha Goldman Sachs Research kimekadiria kuwa kitazidi dola bilioni 700.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...