Na Patricia Kimelemeta
TAASISI ya Chakula na Lishe (TFNC) imefanya utafiti wa utengenezaji wa sampuli za vyakula vya nyongeza kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi sita hadi miezi 59 ili kuhakikisha watoto hao wanakula vyakula bora vyenye kujenga mwili na kuwaepusha na magonjwa.
Akizungumza hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe ( TFNC), Dk. Germana Leyna amasema kuwa utafiti huo umesaidia kupata sampuli tano zilizofanyiwa utafiti ambapo kati ya hizo, sampuli mbili zimefanyiwa tathmini na kukubalika kwa jamii na watoto wenyewe.
"TFNC ilifanya utafiti wa utengenezaji wa sampuli za vyakula vya nyongeza kwa watoto wenye umri wa miezi sita hadi 59, lengo ni kuhakikisha kuwa, watoto wa umri huo wanakula vyakula bora vyenye virutubisho vyote na ambavyo vitawasaidia kuwajenga katika ukuaji wao kwenye malezi na makuzi, kuanza ngazi ya awali," amesema Dk. Leyna.
Ameongeza kuwa mpaka sasa Utafiti huo umefikia hatua nzuri na kwamba na wameweza kutengeneza sampuli tano ambapo kati ya hizo sampuli mbili zimependekezwa na jamii na kukubalika kwa watoto wenyewe zitagawiwa kwa wajasiliamali ili waweze kutengeneza kwa njia ya kuuza au kutoa elimu kwa wazazi na walezi waweze kuwatengenezea watoto wao majumbani.
Amesema kuwa, lengo ni nyongeza uzalishaji wa sampuli hizo na kuzisambaza kuwa wananchi wengine zaidi ili waweze kuzitumia kwa kuwalisha watoto wao, jambo ambalo linaweza kupunguza udumavu pia.
Amesema kuwa, ikiwa mtoto atapewa vyakula bora vyenye virutubisho vyote vitamsaidia kukua vkzuri kiwmili na kiakili na kumuepusha na magonjwa ya mara kwa mara ambayo yanaweza kumrudisha nyuma.
Ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa, qatoto wanapewa vyakula hivyo kwa ajili ya kusaidia kwenye makuzi na malezi yao huku wakiendelea kunyonya maziwa ya mama.
"Watoto ni hazina ya kesho, hivyo basi wanapaswa kulelewa vizuri kuanzia wakiwa wachanga hadi wanapokua ili wawe na afya bora ambayo itasaidia kuimarisha mfumo wao wa ubongo katika ukuaji," amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe ( TFNC), Dk. Germana Leyna
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...