Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

KUFUATIA agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  la kutaka Wizara, Mashirika na taasisi  za serikali kulitumia Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa ustadi mkubwa.

Kauli hiyo ilitolewa wakati wa Uzinduzi wa Huduma pamoja (One Stop Centre) alipozitaka taasisi hizo kutumia huduma ya usafirishaji inayofanywa na Shirika la Posta pindi wanapohitaji kutuma vifurushi au kuhamisha Ofisi zao.

Katika kutii agizo hilo, Taasisi ya BRELA imeanza kutii agizo hilo baada ya kuamua kutumia magari makubwa ya Shirika la Posta kuhamisha Ofisi zao kutoka jengo la Ushirika Mnazi Mmoja na kuhamia ilipokua Jengo la Magereza Posta.

Akitoa taarifa hiyo, Kaimu Meneja Mkuu wa Uendeshajji Biashara Constantine Kasese amesema  Shirika la Posta limepokea kwa mikono miwili kazi hiyo kutoka BRELA na litafanya kwa ufanisi mkubwa ili kuvutia zaidi na taasisi zingine ziwezw kuwahudumia.

Kasese amesema, Magari yao yana uwezo na ni makubwa yanayoweza kubeba mizigo mikubwa na kwa uaminifu mkubwa.

Zoezi hilo la kuhamisha ofisi ya BRELA imeanza rasmi na amewakaribisha taasisi za serikali, kampuni binafsi kutumia Shirika la Posta sababu wanatoa huduma zilizo bora na ufanisi mkubwa.

Magari ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) yakipakia vifaa, nyaraka na vitu mbalimbali kutoka ofisi ya BRELA Jengo La Ushirika Mnazi Mmoja na kuwahamishia katika Jengo la Magereza Posta. Zoezi hilo linatekelezwa na TPC kufuatia Agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzitaka taasisi, Mashirika na Wizara kutumia Shirika la Posta katika kusafirisha nyaraka na mizigo.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...