Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
WAZAZI
na walezi ,wameaswa kuacha kuhusisha watoto kwenye migogoro ya
kifamilia pale inapotokea, kwani watoto hao bado hawana uwezo wa kubeba
mambo ya kifamilia na masomo kwa wakati mmoja ,hali inayosababisha
kuyumba kitaaluma.
Pia wametakiwa ,kupunguza ubize na kufuata majukumu yao ya malezi ikiwa Ni pamoja na kuwafuatilia muenendo wa masomo yao.
Rai
hiyo ,ilitolewa na meneja wa shule za Kibaha Independent (KIPS) pamoja
na Kibaha Annex , Nuru Mfinanga ,wakati wa mahafali ya 16 KIPS na Annex
ikiwa ni mahafali ya kwanza ya kuwaaga wahitimu wa darasa la saba mwaka
2021 wapatao 107.
Nuru alisema ,kwa kuhusisha mambo ya migogoro ya kifamilia majumbani inawaharibu watoto kisaikolojia.
"Tunachanganya
watoto kisaikolojia, mwanafunzi akiwa darasani anakuwa na mawazo yaani
hayupo darasani kabisa ,na ukimfuatilia mtoto wa aina hii lazima
utakuta hafanyi vizuri kimasomo"alisisitiza Nuru.
Mwenyekiti
wa shule hizo, alhaj Yusuph Mfinanga, ameeendelea kutoa kilio chake Cha
kuanzisha sekondari japo kuwa nia hiyo imekuwa ikikabiliwa na
vipingamizi mbalimbali .
Alisema
,walishanunua shule ya Pwani sekondari kupitia mnada wa mahakama na
matarajio ni kuigeza kuwa KIPS sekondari lakini kukatokea vizuizi kwa
takriban miaka mitatu sasa.
"Tumekaa
vikao ,tumeona fedha yetu tuliyonunulia hairudishwi ,na shule hiyo
wameinunua ikiwa haina hati hivyo wameamua kuendelea na mchakato wa
vibali vya kujenga na usajili ili mwakani shule ianze kutoa elimu
"alisisitiza Mfinanga.
Awali
mzazi , Abubakari Alawi alieleza, serikali ya awamu ya sita inajitahidi
kuboresha mazingira bora ya elimu ,Anatoa wito kwa halmashauri kuanza
maandalizi ya miundombinu mapema ili wanafunzi zaidi ya milioni moja
2021,wanaotarajia kuingia kidato cha kwanza mwakani waingie darasani .
"Sio
inafikia muda wa kuingia kidato cha kwanza ndio halmashauri
zinakimbizana kuchimba msingi wa ujenzi ,lakini naimani serikali ipo
imara kwa kuwajengea mazingira mazuri watarajiwa":;'aliongeza Alawi.
Nae
mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri akiwakilishwa
taarifa yake na ofisa tawala wilaya ,Asia Mwinyihaji alisema elimu
waliyoipata wahitimu hao ,ikafungue milango ya maisha yao.
Aliwahakikishia wamiliki wa shule hiyo ,kuwapa ushirikiano katika changamoto zitakazowakabili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...