MWENYEKITI Wa Chama cha Mapinduzi (CCM,) jijini Ilala Ubaya Chuma amesema kuwa, katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu itakayomsaidia katika kujikimboa kiuchumi kwa kushirikiana na madiwani wa jimbo hilo watashirikiana na chuo cha Maendeleo ya Viwanda, Ujuzi na Ubunifu cha Furahika Education College kwa kuwahimiza wazazi na mabinti kujifunza kozi mbalimbali zinazotolewa bure na chuo hicho.

Akizungumza katika mahafali ya nane ya chuo hicho Ubaya amesema, atashirikiana kwa ukaribu na madiwani wa jimbo na Wilaya zote za Mkoa huo katika kuhakikisha chuo kinapata wanafunzi wa kutosha pamoja na walimu ili kuweza kuwafikia watoto wa kike wengi zaidi.

"Kupitia madiwani naamini jambo hili tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa, nawaomba wawakilishi wa madiwani mliopo hapa, mkayafikishe haya kwa jamii, elimu inatotolewa bure kwa mabinti zetu na uhakika wa kupata ajira upo." Amesema.

Aidha amesema, wazazi na walezi wawasaidie walimu katika suala la maadili kuanzia nyumbani ili kujenga vijana imara kwa taifa na jamii kwa ujumla.

"Nimekubali kuwa mlezi wa chuo cha Furahika, wazazi na walezi tushirikiane katika hili ili na kuepusha changamoto tunazoweza kuzikabili ikiwemo mimba za utotoni na nyendo zisizofaa." Ameeleza Ubaya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Chuo hicho Sound Kassim amesema chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo mbalimbali bure kwa watoto wa kike ikiwemo ualimu, ufundi, mafunzo ya hoteli, kompyuta, muziki naa lugha za kigeni ikiwemo kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kichina na kuwataka madiwani kupeleka fursa hizo katika kata zao ili mabinti hao waweze kupata mafunzo hayo yatakayowasaidia kujikimboa kiuchumi

Aidha amesema kuwa malipo yanayochangiwa na wanafunzi hao ni ada ya mtihani wa taifa pekee, huku masula ya chakula na malazi kwa baadhi ya wanafunzi yakisimamiwa na chuo hicho kupitia ufadhili.


Mwenyekiti wa CCM Jiji la Ilala Ubaya Chuma akikabidhi vyeti kwa baadhi ya wahitimu wa kozi mbalimbali za ujuzi na ubunifu zinazotolewa na chuo cha Furahika Education Collage mkoani Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi wa chuo cha Furahika Education Collage Soud Kassim akizungumza wakati wa mahafali hayo na kueleza kuwa mafunzo hayo ni bure kwa watoto wa kike katika kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.


Baadhi ya Madiwani wakiwa katika mahafali hayo.
Mwenyekiti wa CCM Jiji la Ilala Ubaya Chuma akizungumza wakati wa mahafali hayo na kuwataka wazazi na walezi kutumia fursa hiyo kwa kuhakikisha mabinti wanapata elimu, ujuzi na maarifa bure  kutoka chuo hicho.

Baadhi ya wazazi na walezi wakiwa katika mahafali hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...