Waumini wa Dini ya kiislamu Kata ya Kabindi Wilayani BiharamuloMkoani Kagera wamewaomba wahisani kuwasaidia ujenzi wa msikiti mpya baada ya msikiti wa zamani kuharibika na kuhatarisha usalama wao wawapo ibadani.

Ombi Hilo limetolewa na Sheikh Ahmad Bilali ambaye ni Sheikh wa Kata hiyo Sept 10, mwaka huu baada ya kupokea Mifuko 20 ya Saruji iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Mhandisi Ezra Chiwelesa aliyoiahidi kwenye Baraza la Idd.

Bilali amemshukuru mbunge huyo na kumuombea kwa Mungu kwa kuweza kutekeleza Ahadi yake maana amekuwa tofauti na watangulizi wake waliokuwa wakiahidi na hawatekelezi.Ameeleza kuwa kitendo kilichofanywa na Mbunge huyo tangu awe na uwezo wa kutambua alikuwa hajawahi kukiona maana wamekuwa wakiomba misaada mbalimbali hasa kwa viongozi wa kisiasa na walichokuwa wakiambulia ni ahadi hewa.

Kuhusu msikiti kuharibika Sheikh huyo ameomba wadau na wahisani wengine kusaidia kwa kile alichodai kuwa wanapoelekea katika kipindi Cha mvua Kuna uwezekano mkubwa wa kutofanya ibaada msikitini hapo.

“Msikiti wetu kama mnavyouuona kwa nje unaonekana imara ila ukiingia ndani utaona maajabu, na sasa tunaingia katika kipindi cha mvua na mara nyingi inaponyesha mvua huwezi hata kujigama humo ndani hivyo mvua zikianza ibaada itafungwa msikitini hapa.” Amesisitiza Sheikh Bilali.

Aidha amewomba wadau wa maendeleo kuiga mfano aliouonyesha Mhandisi Ezra wa kujitolea kujenga nyumba za ibaada maana ukisha wekeza kwenye nyumba ya kumuabudia Mungu basi wema wako utalipwa hadi siku ya mwisho.

Akiongea baada ya kukabidhi Saruji hiyo katibu wa mbunge Mashaka Maduka ameeleza dhamira ya Mbunge Chiwelesa kuwa ni kuhakikisha analeta maendeleo kwa wananchi wote wa Biharamulo bila kujali  dini wala makabila yao, huku Mwenyekiti wa Ccm Biharamulo Robert Malulu akawaomba waumini hao kuendelea kumuombea Dua njema Mbunge wao.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...