Na. Angela Msimbira TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameielekeza Tume ya Utumishi wa waalimu nchini  kuhakikisha wanafanya msawazo wa waalinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa  ili kuweka uwiano sawa wa waalimu nchini.

Akiongea na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa waalimu Jijini Dodoma Waziri Ummy amaesema kumekuwepo na changamoto kubwa kwa baadhi ya shule kuwa na waalimu wengi huku nyingine zikikosa waalimu, hivyo  ni wajibu wa tume kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa kwa wakati

Waziri Ummy amesema kuna baadhi ya shule zina watoto wengi lakini waalimu ni wachache huku shule nyingine zikiwa na waalimu wengi wanafunzi wachache, ni vyema kukawa na uwiano ulio sawa katika shule zote nchini.

 “Tunafahamu kuwa zipo shule ambazo zinawaalimu wachache hasa maeneo ya vijijini, lakini nyingine zinawaalimu wengi, suala hili halikubaliki, suala hili linahitajika kufanyiwa kazi ingawa mara nyingi serikali inaangalia idadi ya wanafunzi “amesisitiza Waziri Ummy

Waziri Ummy ameendelea kueleza kuwa kutokufanya msawazo hatuwatendei haki wanafunzi walioko vijijini hasa katika maeneo ya pembezoni ni wajibu wa tume kuhakikisha shule zote zinakuwa na idadi sawa ya waalimu

Aidha amewaelekeza Tume ya Utumishi wa Waalimu nchini kutumia mifumo ya kielektroniki katika kutatua kero za waalimu nchini ili kupunguza changamoto hizo kwa haraka na kutoa mrejesho kwa waalimu kwa wakati



 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...