Mtendaji kutoka Taasisi ya TONY BLAIR Eden Gatachew akimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuyafanyia kazi mapendekezo yaliotolewa na serikali kwa lengo la kuimarisha mikakati ya kiutendaji ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwapongeza watendaji wa Taasisi ya TONY BLAIR juu ya misaada mbali mbali inayotolewa na Taasisi hiyo katika kuimarisha sekta mbalimbali.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza taasisi ya TONY BLAIR kwa kazi nzuri inayoifanya kutokana na michango na misaada ya kimaendeleo wanayoitoa kupitia sekta mbali mbali.
Mhe. Hemed alitoa pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na watendaji wa taasisi hiyo waliofika Ofisini kwake Vuga kwa ajili ya kubadilishana mawazo.
Makamu wa Pili wa Rais alisema Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar inaidhishwa na Jitihada zinazochukuliwa na taaisi ya TONY BLAIR inayosaidia sekta tofauti ikiwemo Afya, Miundombinu ya mawasaliano pamoja na masuala mengine ya kijamii.
Makamu wa Pili wa Rais aliwaeleza watendaji hao kuwa, kwa sasa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Rais Dk. Mwinyi katika kuimarisha uchumi wake imelekeza nguvu zake kupitia sekta ya uchumi wa Buluu unaojumuisha mambo mbali mbali kama vile uvuvi, Utalii pamoja na Nishati ya Mafuta na gesi.
Akizungumzia juu ya suala hilo la ukuuzaji wa Uchumi Mhe. Hemed aliomba taasisi hiyo kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuwawezesha wananchi na watendaji wake kwa kuwapatia mafunzo yatakayosaidia kuwajengea uwezo.
Aliwaomba watendaji hao kutoka taasisi ya TONY BLAIR kutoa kipaumbele maalum kwa ajili ya kuimarisha sekta ya Utalii pamoja na sekta nyengine kwa kuweka mifumo itakayounganisha baina sekta moja na nyengine ili kujenga mfumo imara wa kuimarisha utendaji wa kazi za kila siku.
Alifafanua kwamba, kufanikiwa kwa kuimarisha mifumo ya utendaji kazi itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto tofauti ikiwemo kutatua changamoto ya ajira kwa vijana.
Pia Alisema, serikali ya mapinduzi Zanzibar imedhamidhiria kuimarisha sekta ya usafiri kwa kuimarisha Bandari zake na viwanja vya ndege pamoja na kuimarisha uwekezaji kupitia ujenzi wa Viwanda.
Nae Mtendaji kutoka Taasisi ya TONY BLAIR Eden Getachew alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba kupitia mazungumzo hayo na vipaumbele alivyovieleza taasisi ya TONY BLAIR itayafanyia kazi mapendekezo yaliotolewa na serikali na kuangalia namna bora kwa ajili ya utekelezaji wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...