KATIKA kuhakikisha mtoto anapata elimu bora, Uongozi wa Shule za Atlas zimeandaa mbio zitakazohusisha zaidi  ya watu elfu 2000  ili kusaidia kulipia ada za wanafunzi waliopoteza wazazi wao wakati wa Mlipuko wa ugonjwa wa Uviko 19.

Mbio hizo zitajulikana kama Atlas  School half  Marathon  2012  inayotarajiwa kuanza Oktoba 14  mwaka huu zikihusisha mbio za Km21, Km 10 na Km 5.

Katika kufanikisha mbio hizo, Atlas wamekuja na Kauli mbiu inayosema ‘Kimbia kizalendo changia elimu kwa watoto wasiojiweza’

Akizungumza kuelekea mbioz hizo, Mkurugenzi wa shule ya Atlas  Sylivanus Rugambwa amesema baada ya shughuli ya marathon kukamilika watakuwa na sherehe za mahafali ya 19 ya shule zao za msingi Atlas Madale na Ubungo,Atlas Sekondari na Shule za awali.

"Tunategemea kuwa na idadi kubwa ya watu zaidi ya elfu kumi na tano ambao watashiriki katika mahafali hayo katika kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kamati imejiandaa vyema pamoja na watendaji wake ili kunogesha sherehe hiyo za mahafali na marathon,”

Amesema lengo kubwa la kufanya mbio hizo ni kuchangia  watoto wanaosoma katika shule hiyo ambao wazazi wake walifariki kuanzia mwaka jana kutokana na ugonjwa wa Uviko 19.

Rugambwa amesema, hawataki kuona watoto hao wanakosa elimu bali wanahitaji kuendelea kusoma na kupata elimu bora katika kipindi hiki ambacho wamepoteza wazazi wao.

Aidha, Ameongeza kuwa katika kuhakikisha mbio hizo kamati ya utendaji imeandaa siku ya jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi siku ya ukaguzi wa njia ya wakimbiaji ambao watapenda kushiriki watakagua pamoja na njia ya 5km,10km na 21km itakayotumika siku ya Atlas Half Marathon.

Ameongeza kuwa katika mbio hizo mgeni ramsi anatarajiwa kuwa Waziri Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa pamoja na Mkuh wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe sambamba na wageni mbalimbali katika mbio hizo.

"Tunategemea mbio zetu zitahughuliwa na watu mbalimbali  wakiwemo wazazi,watoto,wanafunzi mbali mbali wakimbiaji nguli,wakimbiaji wa kawaida  pamoja na makundi maalum,watu mashuhuri viongozi wa serikali" amesema

Rugambwa amesema,  kuwa zoezi la usajili wa mbio hizo bado unaendelea katika shule zao  Madale  na Ubungo kwa kulipia namba 5927380 pamoja na kituo cha mlimani City  kuanzia muda wa saa 2 asubuhi na jioni ya saa 12.

Hata hivyo katika mbio hizo  mshindi wa  kwanza katika mbio za km 21 350,000 ,kilometa 10Km 200,000,5Km100,000.

Mshindi wa pili ni KM21 ni 300,000,10Km ni175,00 5Km ni 75,000,huku mshind  wa tatu ni 21km 200,000,10km 150,000,5Km50,000.

Mshindi wa nne kwa Km 21 ni 150,000, 10Km 10,000,5Km25,000 huku mshindi wa tano 21 Km 100,000 10Km 50,000 huku 5Km15,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...