Bidhaa mbalimbali za Tanzania zitaanza kutangazwa na kuuzwa kupitia E-COMMERCE PLATFORM ya JD.COM nchini China. 

 

Fursa hiyo ya bidhaa za Tanzania kutangazwa na kuuzwa katika mtandao wa MTANDAO WA JD.COM imetokana na Makubaliano yaliyosainiwa leo jijini BEIJING baina ya Ubalozi wa Tanzania na Kampuni ya PRESTIGE ya CHINA.

 

Mtandao wa JD.COM ni miongoni mwa mitandao maarufu inayoongoza katika mauzo ya bidhaa nchini China ikiwa na watumiaji milioni 700.

 

Katika makubaliano hayo, makampuni ya Tanzania yanayozalisha bidhaa za aina mbalimbali zilizoongezewa thamani yataweza kuuza bidhaa hizo moja kwa moja katika soko la CHINA kupitia mtandao wa JD.COM.  

 

Mbali na fursa ya kutangaza bidhaa za Tanzania katika soko la China, Makampuni yatakayoshiriki kwenye mpango huo yatanufaika na msamaa wa kodi ya kuingiza bidhaa (Import Duty) na punguzo la asilimia 30 katika Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) endapo yatatumia program ya  JD Wordwide Cross Border E-Commerce.

 

Kwa Upande wake, Balozi Kairuki ameishukuru kampuni ya PRESTIGE na JD.COM kwa fursa hiyo ambayo itazidi kulifungua soko la China kwa bidhaa za Tanzania.  Balozi ameyataka Makampuni ya Tanzania yenye nia ya kuchangamkia fursa hiyo yajipange vizuri kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa zilizoongezwa thamani pamoja na kukidhi masharti ya viwango vya ubora katika utayarishaji na ufungashaji wa bidhaa kulingana na sheria za forodha za China.  Bidhaa zinazoweza kuuzwa kutumia Jukwaa hilo ni pamoja na madini (vito) na  vyakula (korosho, kahawa, chai).





 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...