CHUO Cha Elimu ya ujuzi na viwanda cha Furahika Education College kinachotoa mafunzo bure kwa watoto wakike kimeeleza azma yake ya kuendelea kuwapokea watoto wa kike na kuwapa mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuwakomboa kiuchumi pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa chuo hicho David Msuya amesema, chuo hicho kinafadhiliwa na kimesajiliwa na VETA na wanachofanya ni kutoa mafunzo hayo ikiwemo ushonaji, udarizi, udereva, urembo, muziki, mafunzo ya hoteli, kompyuta na lugha za kigeni na mara baada ya kuhitimu wanafunzi hao wanatunukiwa vyeti vinavyotambulika na Serikali na kuingia katika soko la ajira aidha kwa kuajiriwa na kujiajiri wenyewe.

Msuya amesema, Halmashauri za Wilaya, wazazi na walezi washirikiane na kuwahimiza mabinti kupata mafunzo hayo yatakayowasaidia kuwakomboa kiuchumi pamoja na kuepukana na changamoto ya mimba za utotoni.

Kuhusu usajili wa wanafunzi chuoni hapo Msuya ameeleza, fomu za kujiunga zinapatikana chuoni, Buguruni Malapa na katika website ya chuo ya chuoeducationmaendeleo@gmail.com na kuwataka wanufaika kutoka mikoa na halmashauri mbalimbali kutumia fursa hiyo.

Aidha amesema katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wameitumia kutoa mafunzo kwa wanafunzi juu ya mchango wa Baba wa Taifa katika Taifa na nini wafanye kwa kushirikiana na Serikali katika kujenga Taifa imara zaidi.

Vilevile amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuchangia taulo za kike kwa mabinti hao pamoja na bima za afya  ambapo hadi sasa chuo hicho kimeweza kutoa bima za afya kwa wanafunzi 10 pekee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...