Na Mwamvua Mwinyi, Mwanga

MKUU wa wilaya ya Mwanga , Kilimanjaro Abdallah Mwaipaya amesema ni jukumu la wazazi kusimamia muenendo wa watoto wao shuleni badala ya kuwaachia walimu pekee.

Aidha amewaasa wanafunzi kujiepusha kujiingiza kwenye mkumbo wa magenge yasiyofaa ili kulinda hazina ya taaluma waliyoipata kuanzia hatua ya msingi hadi Sekondari.

Akizungumza na wahitimu 74 wa mahafali ya Saba ,ya kidato Cha nne ,walimu na wazazi wa shule ya sekondari ya Vuchama ,Ugweno Islamic iliyopo Mwanga ,mkoani Kilimanjaro aliipongeza shule hiyo kwa namna inavyopika wanafunzi kitaaluma hasa kwenye masomo ya sayansi.

"Dira mliyoionyesha najivunia kuwa na shule ya aina hii wilayani hapa, Ni shule inayohitaji ushirikiano mkubwa kwa wazazi ili iendelee kutoa elimu bora na kuwapa molari wa kufundisha kwa walimu"

Pamoja na hilo , Mwaipaya aliunga mkono ujenzi wa uzio wa shule hiyo kwa kuchangia mifuko 20 ya saruji na kiasi Cha sh.500,000 .

Katika hatua nyingine, Amina Mvungi na Bakari Bashari Hamza Mfinanga ni wanafunzi wa kidato Cha nne waliiongoza kitaaluma 2020/2021 ambapo ameahidi kuwa sehemu ya mahitaji ya wanafunzi hao endapo watafaulu kwenda kidato Cha tano .

Nae Meneja wa shule ya Vuchama Sekondari, Yasin Mfinanga aliiomba serikali ya awamu ya sita ,chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kusaidia kuanzisha chombo cha pamoja Cha kusimamia Serikali na Sekta binafsi katika usimamizi wa elimu .

"Changamoto inayowakumba sekta binafsi ni upatikanaji wa wanafunzi unakuwa mgumu ,Serikali ikaangalia hili kwa kushirikisha kutupatia wanafunzi wanaofaulu kwani na sisi tunaweza kuwaendeleza ,tudumishe ushirikiano uliopo"alisisitiza Yasin.

Awali mkuu wa shule hiyo ya Sekondari Jumanne Mkoga alieleza, shule hiyo inafanya vizuri katika ufaulu wa kidato Cha nne miaka mitano mfululizo.

Alitaja changamoto ya uzio na kuomba watu wajitolee kumaliza changamoto hiyo ambapo wanahitaji mifuko ya saruji 22,100, roli za mchanga 195 kwani kwa kufanikisha ujenzi huo itasaidia kulinda Mali na ulinzi wa wanafunzi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya wadhamini ya shule ,alhaj Yusuph Mfinanga aliwataka, wazazi na walezi wafuatilie muenendo wa masomo ya watoto wao wakiwa shuleni .

Mfinanga aliwataka na wahitimu pia, kwenda kuendeleza taaluma waliyopata na kujiepusha kutumia muda watakaokuwa nyumbani kujiingiza kwenye mambo yasiyo na maadili hasa bangi ,na vishawishi vya ngono .

Hata hivyo alihimiza ,jamii kuchanja chanjo ya UVIKO19 ili kujikinga na ugonjwa wa Corona .

Akizungumza kwa niaba ya wahitimu Amina Ndosi alieleza ,shule hiyo imewafunza nidhamu ,maadili mema ikiwemo namna ya kujistiri .

Alisema wanaipongeza shule kwa utekelezaji wa taaluma na falsafa nzuri ya ufundishaji .




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...