Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Philip Isdor Mpango
amewaagiza wakuu wa mikoa inayomwaga maji mto Rufiji kudhibiti uchafuzi
wa mazingira katika bonde la mto huo, ili kulinda ujenzi wa mradi
mkubwa wa umeme katika bwawa la Mwalimu Nyerere -Rufiji,uliofikia
asilimia 48.
Amewaagiza
wakuu hao wa mikoa ikiwemo Pwani na Morogoro, kuchukua hatua kwa wale
wote wanaochoma misitu ovyo, shughuli zinazohatarisha mazingira pamoja
na mifugo holela.
Akizungumza
wakati alipotembelea mradi wa bwawa la kuzalisha umeme -stigo Rufiji
ambalo litazalisha umeme Megawatt 2115 ,Mpango alieleza wakuu wa mikoa
hiyo ikiwemo Pwani na Morogoro wadhibiti changamoto hizo ili mradi uweze
kuwa na maji ya kutosha .
"Mshughulikie
hili bwawa ni zuri tusiriharibu ,Nina taarifa kuna jitihada mnazichukua
kudhibiti hali hii ,lakini ongezeni nguvu kuwa mazingira safi "
Bwawa
hili lina faida kubwa kwa watanzania ,tunataka umeme wa kutosha nchini
,utalii na umwagiliaji,hivyo tulinde mazingira na kudhibiti uchafuzi wa
mazingira,"alifafanua Mpango.
Mpango
alibainisha ,ana wasiwasi Kuna uchomaji holela ,wasimamie hili kulinda
Kodi ya watanzania ndio wanachangia Kodi na kusababisha miradi hii
mikubwa kuleta maendeleo na kuinua uchumi.
"Nimeona
leo mlale na agizo hili, kwakuwa umeme ni kila kitu,Mimi ndio msimamizi
wa mazingira nisipoona mnalisimamia nitatumia rungu jingine "
Aidha
Mpango amewaelekea mainjinia waongeze wafanyakazi na endapo wakiona
changamoto za mradi kuhakikisha wanazitatua kwa wakati.
Pamoja
na Hilo,aliwapongeza vijana wa kitanzania waliopata ajira kwenye ujenzi
huo ,kwenda sambamba na teknolojia mpya za kujenga ujenzi wa miradi
mikubwa na amewataka wawe mfano wa kuigwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...