Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkazi wa Ngara, Bukoba Expectance S. Gwomeka ameibuka mshindi wa bonasi ya Jackpot ya wiki iliyopita kutoka SportPesa ambapo alibashiri michezo mbalimbali ya jackpot na kufanikisha kwenye bashiri moja kwa kupata TZS 21,191,497 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13.

Akizungumza wakati wa mahojiano ofisi za Sportpesa, Expectance alisema “Mimi ni mfanyabiashara na vilevile ninajishughulisha na kilimo kama sehemu inayoniingizia kipato.

“Ni muda kidogo tangu nianze kubashiri kwani nilikuwa nikihamasishwa na baadhi ya washindi waliopita wa bonasi lakini hasa ni washindi wa Jackpot ambao wameweza kushinda milioni 300, 400. Nikaona na mimi nianze kucheza huenda siku nitashinda”

“Pesa niliyoipata itaenda kuendeleza kilimo na kuboost biashara moja kwa moja kwani kule kwetu sasa hivi ni msimu wa kupanda mahindi, maharage kwahivyo hii pesa imekuja muda muafaka”.

“Nawasihi wapenda michezo wazidi kujiongeza na kuanza kubashiri na SportPesa kwani baada ya mechi kuisha kama utaibuka mshindi utawekewa pesa zako kwenye akaiunti ya Sportpesa moja kwa moja”

Kwa upande wa SportPesa Meneja Uhusiano Sabrina Msuya alisema bashiri ni moja kati ya aina ya burudani na ndiyo maana kila wiki tunakuletea Jackpot mpya na mechi za kukusisimua kama moja ya  kivutio cha Jackpot.

Amesema, “Jackpot ya wiki hii imefika Tsh. 576,086,780 inakusubiri wewe uweze kubashiri mech izote 13 kwa usahihi ili uweze kuwa milionea mpya wa Sportpesa.”
Mkazi wa Ngara, Bukoba Expectance S. Gwomeka akizungumza baada ya kunyakua kitita cha Shilingi TZS 21,191,497 baada ya kubashiri kwa usahihi michezo 12 kati ya 13 katika jackpot.
Mkazi wa Ngara, Bukoba Expectance S. Gwomeka akizungumza baada ya kunyakua kitita cha Shilingi TZS 21,191,497 baada ya kubashiri kwa usahihi michezo 12 kati ya 13 katika jackpot.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...