Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

JIMBO  la Musoma Vijijini ambalo Mbunge wake ni Prof Sospeter Muhongo, limekuwa kinara wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ya mwaka 2020-2025.

Mafanikio ya Jimbo hili yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya Wanavijiji, Viongozi wao na Serikali yetu. Wanavijiji na viongozi wao, akiwemo Mbunge wa Jimbo, wamekubali kuchangia nguvukazi na fedha taslimu kwenye utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo.

Kwa saaa Jimbo la Musoma Vijijini limepata Sh.Milioni 500 za COVID-19 kwa ajili ya kusambaza maji vijijini  kutokana na mapendekezo ya Mbunge wa Jimbo.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini kwa vyombo vya habari leo Oktoba 24 ,2021 imefafanua kuhusu matumizi ya fedha hizo kwa katika jimbo wamepanga kujenga tenki la maji la mita za ujazo 200 (lita 200,000) Mlimani Nyaberango, Kijijini Nyambono, Usambazaji wa mabomba ya maji kutoka kwenye tenki hilo kwenda Vijiji vya Kanderema ,Bugoji na Kabirabura.

Imeelezwa kuwa Mlimani Nyaberango (Kijijini Nyambono) tayari lipo tenki la maji  (200 cu.m./lita 200,000) kwa ajili ya maji vijiji vya Saragana , Nyambono na Mikuyu.Tenki hilo limejengwa kwa kutumia Fedha za Bajeti za Mwaka 2019/2020

Pia imesema chanzo cha maji ya bomba ya vijiji sita , katika fedha za Bajeti ya Mwaka 2019/2020 na Mwaka 2020/2021 zimewezesha ujenzi wa Miundombinu ya kutumia Maji ya Ziwa Victoria kutoka kwenye chanzo kilichopo Kijijini Suguti.

"Maji ya kutoka Kijijini Suguti  yanapelekwa hadi Kijijini Chirorwe ambapo mabomba yametandazwa kupeleka maji Kijijini Wanyere na mengine kupeleka maji, kupitia Mlima Nyaberango, kwenda Vijijini Saragana ,Nyambono na Mikuyu."

Wakati ombi la wanaviji vyote sita wanaombwa kurahisisha upatikanaji wa maeneo ya kutandaza mabomba ya kusafirisha maji yatakayo kuwa kwenye matenki mawili Mlimani Nyaberango.Wanavijiji wanaombwa kuchangia nguvu kazi kuchimba mitaro ya kutandaza mabomba ya maji na kwamba wajitolee na  wachangie upatikanaji wa maji ya bomba katika vijiji hivyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa mradi huo umepangwa imepangwa ifikapo Desemba 30 2021, maji ya bomba  yaanze kutumika ndani ya vijiji vya Mikuyu, Nyambono, Saragana,Kanderema,Bugoji na Kaburabura.

Kutokana na mpango huo shukrani za dhati zimetolewa na Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kwenda kwa Serikali ya Awamu ya Sita hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha  upatikanaji wa fedha za COVID-19 na nyingine kwa manufaa ya Taifa letu.

 "Booster" iliyojengwa Kijijini Chirorwe kwa ajili ya kupandisha maji  kwenda kwenye yenki lilojengwa Mlimani Nyaberango, ndani ya Kijiji cha Nyambono.
Tenki la Maji (Lita 200,000 - lenye ngazi pichani) ya Vijiji vya Saragana, Nyambono na Mikuyu lililojengwa Mlimani Nyaberango, Kijijini Nyambono

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...