• Michezo ya kubahatisha ya Play & Win katika * 150*88 #

• Zawadi Kabambe za kujishindia

• Tiketi kwa Malipo Kiduchu kupitia HaloPesa au Muda wa Mongezi au HaloPoints

· HaloPoints ni Pointi za Bure Mteja anazojipatia kwa kufanya baadhi ya miamala yake ya kawaida ya HaloPesa


Dar es Salaam, Oktoba 26, 2021 Halotel Tanzania kupitia huduma yake ya HaloPesa, inawaletea wateja huduma nyingine bora inayowapa fursa ya kujishindia zawadi kabambe; HaloPesa leo imeanzisha kampeni ya "PLAY & WIN" kwa wateja wake wote nchini. HaloPesa inakusudia kuwazawadia wateja wake mamilioni ya fedha na zawadi mbalimbali kila siku, kila wiki na kila mwezi kupitia michezo rahisi na shirikishi ya PLAY & WIN iliyopo katika menyu ya HaloPesa kupitia*150*88#.

"HaloPesa zaidi tu ya kuwa huduma ya kifedha, sasa ni Huduma Jumuishi ya Kifedha na Mtindo wa Maisha kwa wateja wetu. Katika mengi yenye ubunifu ambayo tumewezesha, ni pamoja na kuwapa fursa wateja wetu kuweza kununua muda wa maongezi kwa mitandao mingine.

Uzinduzi wa huduma ya PLAY & WIN na Dunia Investment leo, ni hatua nyingine ya ubunifu kutoka HaloPesa kufikisha thamani hiyo ya mtindo wa maisha kwa wateja wetu wote nchini. ”Bwana Magesa Wandwi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa HaloPesa alisema.

PLAY & WIN ni ubia wa kimkakati kati ya Dunia Investment & HaloPesa unaowezeshwa na Axieva Africa, kuzindua aina mbalimbali za michezo ya kubahatisha nchini. Michezo hiyo ni pamoja na Tatu Dodo, Bid2Win, Win X-Multiply, Mega 5,000,000 n.k. Wateja wetu waendelee kucheza na Kutumia huduma zetu bora za HaloPesa na wajipatie fursa ya kujishindia Pesa na Zawadi mbalimbali. Aliongeza Magesa.

Bwana Kobus Schoeman, Mkuu wa huduma na mahusiano kwa wateja wa Dunia Investment- mbia wa huduma ya PLAY & WIN- alisema "Michezo na Burudani ni sehemu asili ya utamaduni wetu wa Kiafrika. Kwa namna moja au nyingine, hakuna siku hata moja ambapo hatuigusi katika Maisha yetu! PLAY & WIN kwa ushirikiano na HaloPesa, inakusudia kuleta utamaduni huo kwenye Simu ya Mkononi.

Iwe ni mteja asiye na ujuzi wa michezo ya bahati nasibu na mwenye shauku au mchezaji anayefahamu na kufurahia michezo ya bahati nasibu, PLAY & WIN utakuwa ni mchezo wa wote. Huduma hii pia inajumuisha watumiaji wa aina zote za simu, na lugha ya Kiswahili.

Tuna hakika kwamba, wateja zaidi wa HaloPesa watafurahia huduma ya PLAY & WIN. Na wateja ambao bado hawatumii HaloPesa, watajiunga ili kufurahia faida za huduma hii.”aliongeza Kobus.

Kitu kikubwa kwenye Kampeni hii ni HALOPOINTS ZA BURE! Kulingana na aina ya miamala, mteja atapewa HALOPOINTS ZA BURE moja kwa moja wakati wowote anapofanya baadhi ya miamala ya HaloPesa. Kulingana na aina ya muamala, mteja anaweza kupata Halopoints kisha kuzitumia kwenye Michezo ya PLAY & WIN. Zaidi ya HaloPoints, wateja pia wanaweza kufanya malipo ya tiketi za michezo hii kwa kutumia HaloPesa au Muda wa maongezi kupitia *150*88 #”.

Naibu Mkurugenzi wa Halopesa Mr. Magesa Wandwi (Kulia), Afisa Mkuu wa Fedha Mr. Kobus Schoeman (Kushoto),wakisaini Mkataba wa Ushirikiano katika Ofisi za makao Makuu ya Halotel wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Pay and Win inayopatikana kupitia Halopesa kwa kupiga *150*88# ambapo wateja wa Halopesa watapata fursa ya kujishindia pesa Taslimu na Zawadi mbalimbali. Wakishuhudia ni Joseph Jackson Mkuu wa Idara ya Biashara Halopesa, na Bhavik Sudesh Solanki Mhasibu wa Kampuni ya Dunia Investment.
Naibu Mkurugenzi wa Halopesa Mr. Magesa Wandwi (Kulia), Afisa Mkuu wa Fedha kampuni ya Dunia Investment LTD Mr. Kobus Schoeman (Kushoto),akiongea na waandishi wa Habari katika Ofisi za Makao Makuu ya Halotel wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Pay and Win inayopatikana kupitia Halopesa kwa kupiga *150*88# ambapo wateja wa Halopesa watapata fursa ya kujishindia pesa Taslimu na Zawadi mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...