BAGAMOYO Kutanoga ! Ndivyo unavyoweza kuelezea kwani Wasanii maarufu nchini pamoja na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajia kushiriki Tamasha la 40 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo,ambapo wasanii hao watatoa burudani.

Maandalizi yote kuhusu tamasha hilo kubwa la kimataifa ambalo linatarajiwa kushuhudiwa na maelfu ya watu linatarajia kuanza Oktoba 28 mwaka huu hadi Oktoba 30,2021 katika Viwanja vya Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TASUBA).

Tamasha hilo ambalo limetambulishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi pamoja na Uongozi wa Mkoa wa Pwani,litakuwa pambe na la aina yake .

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bagamoyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema wizara itahakikisha tamasha hilo kuendelea kuwa kubwa na iwe sehemu ambayo vitu vyote vya asili vipatikana.

Amesema malengo ya Wizara kuendeleza, kuzikuza na kuzifanya sekta za sanaa na tamaduni ziweze kuwa na mchango mkubwa katika Jamii.

"Tamasha hili la Bagamoyo tutaliunganisha na maeneo ya kutangaza utalii kutakuwa na tour mbalimbali za watu kwenda kwenye kutalii lakini kuna siku moja ambapo ni tarehe 30 wasanii watatembelea Saadani". Amesema

Aidha Dkt.Abassi amesema nje ya kuwepo kwa burudani kutoka kwa wasanii kutakuwa pia na maonesho mbalimbali ya sanaa,kutakuwa na vyakula vya kiutamaduni na vitu vingine vya asili.

Amesema kutakuwa na kila aina ya sanaa kama vile maigizo,Uchoraji, Uchongaji, Sarakasi pia kutakuwa na wasanii ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika tasnia hiyo wataweza kutoa burudani za kutosha.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakary Kunenge amewahakikishia washiriki katika tamasha hilo usalama na amani katika kipindi chote cha tamasha hilo litakapokuwa linafanyika.

Amesema wamejipanga vizuri kwani tukio hilo litakuwa ni miongoni mwa matukio makubwa ya kihistoria na kutazidi kutangaza nchi yetu hasa wilaya ya Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani.

Tamasha la 40 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28-30, 2021 limetambulishwa leo Oktoba 26, 2021 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamo (TaSUBa)

Katika utambulisho huo walikuwepo wasanii mbalimbali watakaotumbuiza katika tamasha hilo akiwemo Dulla Makabila, Frida Amani, Ruby, Mrisho Mpoto, Barobaro, Meja Kunta, Isha Mashauzi, Maarifa, Beka Flavour, Saada Nassor na Rapcha.
Bagamoyo hakutaki 'stress' kabisa .Muimbambji nyota wa muziki wa Mwambao Taarab Isha Mashauzi akiwa na Msani mwenzake aitwaye Ruby wakiburudika na juisi freshi kabisa 'maji ya dafu' wakati wa kutambulishwa kwa wasanii mbalimbali watakaotumbuiza kwenye Tamasha la 40 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kuanzia kesho Oktoba 28-30,2021 ndani ya mji mkongwe na wa Kihistoria wa Bagamoyo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakary Kunenge akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari kwenye hafla fupi ya kuwatambulisha Wasanii mbalimbali watakaoshiriki kwenye Tamasha la 40 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28-30, 2021 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassanakizungumza mbele ya Waandishi wa Habari kwenye hafla fupi ya kuwatambulisha Wasanii mbalimbali watakaoshiriki kwenye Tamasha la 40 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28-30, 2021 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt Herbert Makoye akiwatambulisha Wageni waliofika kwenye hafla fupi ya kuwatambulisha Wasanii mbalimbali watakaotumbuiza kwenye Tamasha la 40 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28-30, 2021 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)
MKuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.Zainab Abdallah akiwashukuru wageni waalikwa mbali mbali waliofika kwenye hafla fupi ya kuwatambulisha Wasanii watakaotumbuiza Tamasha la Kimataifa la Sanaa na tamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021.

Mdau mkubwa wa muziki wa Singeli, mtangazaji kutoka kituo cha EFM akieleza ni namna gani muziki huo umefanikiwa kupenye kwenye anga ya muziki wa kizazi kipya na kuonekana kupendwa zaidi

Mmoja wa Wasanii anaekuja kwa kasi katika miondo ya muziki wa Singeli nchini aitwaye kwa jina la kisanii Meja Kunta akionesha umahiri wake wa kuimba mbele ya wageni waalikwa wakati wa kutambulishwa kwao,tayari kwa kupanda jukwaani hapo kesho kwenye Tamasha la Kimataifa la Sanaa na utamaduni Bagamoyo
Mkongwe mwenyewe katika uga wa kughani mashairi kwa namna ya kipekee kabisa,anaitwa Mrisho Mpoto'Mjomba' akijitambulisha kwa ufupi mbele ya wageni mbalimbali wakati wa kutambulishwa kwao tayari kwa kulinogesha tamasha la Kimataifa la Sanaa na utamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 28 hadi 30, 2021.
Msanii wa kizazi kipya wa Hip Hop aitwaye Rapcha kutoka Bongo Records akionesha vionjo vyake vya kughani kwa umahiri mkubwa mbele ya wageni waalikwa walioshiriki mkutano wa kuwatambulisha wasanii watakaoshiriki katika tamasha hilo litakalojumuisha kila aina ya Wasanii na kuufanya mji wa Bagamoyo uwe shangwe tuu.
Mmoja wa waimbaji wa muziki wa Taarabu kutoka Zanzibar nae atakuwepo kutumbuiza kwenye tamasha hilo
Msanii wa Singeli nchini Dulla Makabila akizungumza wakati wa kujitambulisha na kushiriki  Tamasha la Kimataifa la Sanaa na utamaduni Bagamoyo litakaloanza kufanyika hapo kesho Oktoba 28 hadi 30, 2021.
Msanii wa kizazi kipya atambulikae kwa jina kisanii Bekafleva akijitambulisha mbele ya wageni waalikwa kuhusu kushiriki tamasha hilo
Mmoja wa akina Dada machachari kabisa kabisa katika miondoko ya 'Kurap' naye atakuwepo.
Msanii wa kizazi kipya ambaye amejipatia sifa lukuki kwa kuimba nyimbo laini laini aitwaye kwa jina la kisanii Ruby akionesha kipaji chake cha kuimba na namna atakavyowashangaza wakazi wa Mji wa Bagamoyo kwa kucheza na sauti zake laini katika jukwaa la tamasha hilo la Kimataifa latakalowakutanisha wageni malimbali wa ndani wa nje
Mwanamama Mahiri na mwenye kipaji adhimu kabisa cha kuimba muziki wa mwambao 'taarabu',apendae kujitambulisha kwa jina la Kisanii Dume la Simba,Isha Mashauzi akitoa vionjo kadhaa mbele ya wageni waalikwa waliofika kushuhudia kutambulishwa kwao kwa ajili ya kushiriki Tamasha la 40 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kuanzia kesho Oktoba 28-30,2021 ndani ya mji mkongwe na wa Kihistoria wa Bagamoyo.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhe. Mhe.Abubakary Kunenge akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt Herbert Makoye mara baada ya kuisha mkutano wa kuwatambulisha wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo
Majadiliano kidoogo kwenye Meza kuu

Raha ya dafu sasa kutoka Bagamoyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...