KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema Chama hakipo tayari kumfumbia macho mtumishi yeyote wakiwemo wa umma, ambao utendaji wao utakuwa kero kwa wananchi.

Amesema CCM imeahidi kupitia Ilani yake ya Uchaguzi ya 2020-2025 kuwa, itaendelea kuwa daraja la kuwafikisha wananchi huduma bora ili kuchochea kasi ya maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Shaka aliyasema hayo leo Dar es Salaam wakati akiwahutubia mamia ya vijana walioshiriki kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kazi nzuri anayofanya katika kuiongioza nchi ikiwemo kufanikisha kupatikana kwa mkopo wa sh. trilioni 1.3 wa mashtri nafuu, kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

"Chama Cha Mapinduzi (CCM), tunawataka watumishi wote wa umma nchini kuendeleza utendaji kazi wenye weledi, nidhamu na heshima kwa wananchi kwani hao ndio waajiri wa serikali iliyopo madarakani, kwa kulipa kodi na kuiweka madarakani kwa kura zao," alisema Shaka.

Alieleza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan na serikali anayoiongoza wana maono, uthubutu, uzalendo, waumini wa nidhamu ya kazi na matokeo yenye kuchochea ustawi wa wananchi.

Kwa mujibu wa Shaka, CCM inakemea tabia inayoanza kujitokeza kwa baadhi ya watumishi wa umma wa kada mbalimbali, kuzembea na kufanya kazi wa mazoea bila ya kuheshimu wala kuwajali wananchi.

“Siri ya Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuaminiwa na Watanzania kuongoza nchi yetu, ni kwa sababu kinabeba agenda za maendeleo, kinatoa matumaini na suluhu kwa changamoto zinazoikabili jamii,” alisema.

AMPONGEZA RAIS SAMIA

Shaka alisema sera za Rais Samia anazoendelea kuzitekeleza tangu ameingia madarakani, zimetoa mwelekeo chanya wa kuimarisha na kuboresha ustawi wa maisha ya Watanzania katika kila sekta, huku  amani ikipewa kipaumbele. 

"Kitendo cha Mheshimiwa Rais Samia Saluhu Hassan kuamua kuwapatia mrejesho wa kazi za maendeleo ambazo serikali imefanya kwa miezi sita tangu ashike madaraka, ni uwazi na uwajibikaji.

"Chini ya uongozi wa Rais Samia Serikali ya CCM inazidi kujipambanua katika misingi ya utawala bora na demokrasia inapotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya 2020 - 2025, kwa kuzingatia uwazi na uwajibikaji,” alisema.

Shaka alisema ni jukumu la Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kazi nzuri anayofanya ili kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ikiwemo kusogeza karibu huduma mbalimbali za kijamii.

Awali akizungumza katika kongamano hilo, Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, alisema viaja mkoani mwakake, wapo pamoja na Rais Samia na kwamba wataendelea kuwa mstari wa mbele kutekeleza maagizo mbalimbali anayoyatoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...