NA Mwandishi Wetu –
Moshi
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
imejipanga kimkakati kupitia mpango kambambe wa Taifa wa Umwagiliaji wa mwaka
2018, kukabiliana na athari na madhara yatokanayo na mabadiliko ya Tabia nchi
katika sekta ya Kilimo.
Hayo yamesemwa leo mjini Moshi katika maonesho yanayoendelea
kuelekea maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani na Mhandisi Naomi Mcharo,
kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Mhandisi Naomi amesema kuwa,mabadiliko ya tabianchi
yamesababisha ukame na wakati mwingine mafuriko yanayosababisha madhara katika mashamba
na uharibifu wa miundombinu ya umwagiliaji, “ kwa hivyo sisi Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji tuna Mpango kabambe ambao tumeanisha kuanzia miaka 10 mpaka 20 ya
kukabiliana na mabadilio ya Tabia nchi, kwa maana ya kwamba tumepanga kuwa na
Ujenzi wa mabwawa nchi nzima takribani mabwawa 88, ambayo yapo kimakakati
katika maeneo kame.” Alisisitiza.
Aidha, Mhandisi alibainisha kuwa mabwawa hayo yatajengwa
katika maeneo ambayo yanapata ukame kwa muda mrefu na mvua zenye kuleta
madhara.
Alibainisha kuwa, maeneo mbayo yatajengwa na yamejengwa
mabwawa hayo kama vile katika wilaya ya Kwimba yanasaidia kukabiliana na athari
na madhara yatokano na mabadiliko ya Tabia nchi.
Awali Mhandisi Naomi alieleza kuwa, Fedha zinazoingia katika
mfuko wa Taifa wa Umwagiliaji zinatoka katika vyanzo mbali mbali vya mapato,
ikiwa ni pamoja na ukodishwaji wa mitambo inayomilikiwa na Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji, ambapo fedha hizo zinatumika katika kazi ya matunzo, matengenezo na ujenzi wa
Miundombinu katika skimu za kilimo cha umwaguliaji nchini, akitolea mfano wa
ukarabati wa skimu ya Pawaga, na Dakawa
unaoendelea, Ruaha Mbuyuni ambapo ukarabati wa kingo ya mto Lukosi ulioacha
njia umekamilika, na Urumwi Ujenzi unaendelea wa mfumo shirikishi kwa wananchi
yaani force account.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...