Na.Vero Ignatus,Dodoma
Wito umetolewa kwa wakulima Nchini kukata bima ya mazao ili kuepuka hasara ambayo inaweza kujitokeza,kutokana na majanga mbalimbali,yanayowezeza kujaribu mazao yao
Wakulima wameelezwa kwamba bima hiyo ina Kinga dhidi ya madhara mbalimbali yanayotokana na Moto,mabadiliko ya hali ya hewa,mafuriko,pamoja na ndege wanaosababisha hasara kwa kuharibu mazao.
Elieza Rweikiza ni Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini, akizungumza katika maonyesho ya wiki ya posta, aliwashauri wakulima kwenda katika makampuni ya bima yanayo shughulika na bima ya mazoa ili waweze kukata bima hizo.
Aidha Rweikiza alisema kwa Sasa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Nchini (Tira) inayo makampuni 31 ambayo yamekuwa yakitoa huduma za bima mbalimbali
Ameainisha bima hizo ni pamoja na ya kilimo na ufugaji ,ambapo amewataka wananchi watumie fursa hiyo kupata Kinga ya mifugo na mazao yao
Aidha wiki ya posta huadhimishwa kila mwaka octoba 6 ambapo Nchini imefanyika Jijini Dodoma.
Wakwanza kushoto Ni Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini Elieza Rweikiza ,akitoa ufafanuzi wa shughuli za utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mhe.Kundo Andrea Methew (kwanza kulia)katika maadhimisho ya wiki ya posta duniani yaliyofanyika Jijini Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...