RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia SuluhuHassan, ameingia kwenye vifua vya Watanzania wengi, baada ya kuamuakuondolewa kwa tozo za mafuta nchini. Uamuzi huo umetafsiriwa kamasehemu ya kutafuta mwarobaini wa shida za wananchi wengi.
Hata hivyo uamuzi huo umetokana na maoni ya Waziri wa Nishati na Madini,Mheshimiwa January Makamba, aliyefikisha mtazamo wa namna ganiwananchi wanahitaji kupunguziwa makali ya maisha kwa kuangalia jambo nyeti kama tozo za mafuta.
Ni kwa sababu hiyo, Watanzania wanaweza kuokoa zaidi ya sh Bilioni 102 kwa mwaka kutokana na tozo hizo. Kwa kuanza kuangalia kupunguzwa kwa tozo hizo kwa Watanzania, utagundua ni kiasi gani wananchi walikuwa wanabebeshwa mzigo mzito.
Hakuna mwananchi ambaye haguswi na matumizi ya mafuta nchini kote. Kwa mfano, wapo wananchi wa vijijini ambao maisha yao bado yanategemea mafuta ya taa ili wamulike kwa kutumia vibatari vyao.
Ukiacha hao wanaotumia kibatari, bado nauli za kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine ilikuwa ghali, huku wahusika wakisema chanzo cha mzigo huo wa nauli kikiwa ni gharama ya uendeshaji wao, ikiwamo tozo.Mafuta kama diesel, petrol, mafuta ya taa na vilainishi vingine vilichangia kwanamna moja ama nyingine kupanda kwa gharama za maisha, hivyo kwa kushushwa kwake kutapunguza ukali wa maisha.
Ni kawaida kwa wauzaji na watoa huduma wengi kupandisha gharama za bidhaa zao punde baada ya gharama za uendeshaji wao kupanda. Hali hii imekuwa ikiongeza gharama za maisha kwa wananchi wote, wakiwamo masikini wanaoishi vijijini.
Hivyo kwa Rais kuamuru ushushwaji wa tozo hizo, aghalabu wananchi watapumua, maana mzigo wote huo walikuwa wanaubeba wao. Kwa mujibuwa Rais Samia, tozo zinazotakiwa kuondolewa ni pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, Tozo ya Miundombinu, Mamlaka yaMapato Tanzania, tozo ya kuchakata taarifa, Shirika la Viwango Tanzania, tozzo
ya kupima ubora wa mafuta kwenye meli na gharama ya uwekaji wa vinasaba kwenye mafuta.Tozo nyingine ni Wakala wa Vipimo Tanzania, tozo ya uhakiki wa ujazo wamafuta kwenye meli, Wakala wa Usimamizi wa Meli, tozo ya forodha, Mamlakaza serikali za mitaa, ushuru wa huduma kwenye halmashauri nne zenyemaghala ya kupokea mafuta kwa ujumla kama vile Kigamboni na Temeke
mkoani Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.
Inakadiliwa sh 133 kitaokolewa kwa kila lita moja, huku jumla ya tozo nanezikishushwa kutokana na agizo hilo la Rais Samia. Hii ni bahati kubwa kwa Watanzania kuwa na Waziri anayeguswa na shida za watu wengi, Makamba, ambaye kwa kulifanyia kazi jambo hilo akaamua kulifikisha kwa Mheshimiwa
Rais ili alitolee uamuzi.
Huu ni mwendelezo wa kupunguza kero kwa Watanzania. Ikimbukwe mwezi Mei mwaka huu, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ilipunguza pia gharama za uunganishwaji umeme majumbani. Sasa Watanzania watatakiwa kuwa na kiasi sh 27,000 tu ili waunganishiwe umeme kwenye majumba yao tofauti na zamani, ambapo kwa mtu anayehitaji nguzo moja tu ya umeme ilimlazimu awe
na zaidi ya sh 516,000.
Gharama za kuunganishwa umeme wa bei rahisi 27,000 ilikuwa vijijini tu chini ya Wakala wa Umeme vijijini (REA), lakini sasa bei hiyo ya sh 27,000 itawahusuwa Tanzania nzima, mjini na vijijini.
Kama Taifa, nchi inakwenda vizuri. Ni budi kwa Watanzania wote kumuunga mkono Rais wetu kwa sababu ameamua kufanyia kazi kero sugu zilizokuwazinawatoa damu. Sasa ni wazi nauli zitashuka. Wale waliokuwa wanashindwakutembelea wapendwa wao mikoani ni wazi sasa wataenda.
Ikiwa lita moja ya mafuta bila tozo hizo Mtanzania anaokoa sh 133, ni wazi kwa matumizi ya lita 100 tu ya petrol, ataokoa sh 13,300. Fedha hizi ni nyingi zinaweza kutumika kwenye huduma nyingine muhimu za kimaisha.
Tozo ya mafuta ilimgusa kila mtu. Huko vijijini ukiacha wanaotumia vibatari,
bado wakulima walishindwa kuendelea kiuchumi kwa kushindwa kutumia
kilimo kwa kutumia trekta kwa sababu ya wamiliki na waendeshaji wa vyombo
hivyo kuweka gharama kubwa.
Zaidi ya sh 50,000 inahitajika kwa heka moja tu kama mkulima atalazimika
kutumia trekta kulima shamba lake. Kwa heka 5 atalazimika kuwa na sh
250,000. Fedha hizi ni nyingi. Kwa kushushwa kwa tozo hizo kwenye mafuta, ni
wazi wamiliki hao wa trekta nao watashusha bei zao iwe kwa ridhaa zao ama
kwa kuelekezwa na serikali.
Itashangaza kama watoa huduma hao wataendelea kutoza bei zao za zamani,licha ya serikali kuondoa tozo chechefu zilizokuwa zinasababisha makali yamaisha kwa wananchi.
Bahati nzuri Wizara ya Nishati na Madini imepata Waziri ambaye ni mfuatiliaji,hivyo atasimamia maagizo ya Mheshimiwa Rais kwa vitendo. Serikali imechukua uamuzi huo kwa kujua ni mwarobaini wa tatizo la ugumu wamaisha ya Watanzania.
Ni matumaini makubwa ya Watanzania kuwa mtazamo wa Rais Samia pamoja na wasaidizi wake akiwamo Mheshimiwa Makamba itasaidia kuwafanya wananchi wanufaike kiuchumi.
Wale ambao watashindwa kurudi kwenye matamanio ya serikali kwa kushusha bei za bidhaa zao wawajibishwe kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata ahueni ya kimaisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...