Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Bouygues International ya nchini Ufaransa Eric Fleurisson Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mzungumzo hayo Eric amesema kampuni ya Bouygues ina nia ya kuwekeza katika sekta ya Afya nchini hususan katika Ujenzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa mkoani Dodoma. Aidha, amesema kampuni hiyo ina uzoefu kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimataifa katika Bara la Afrika ikiwa imejenga Hospitali katika nchi za Benin, Ghana na Ivory Coast.

Makamu wa Rais , Dkt. Philip Mpango amekaribisha uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini na kuongeza kwamba kutokana na Serikali kuhamia mkoani Dodoma, mahitaji mbalimbali yamezidi kuongezeka hasa katika sekta ya afya. Makamu wa Rais amesema uwekezaji wa ujenzi wa Hospitali yenye ubora na vifaa vya kisasa utaongeza tija kubwa kwa wakazi wa Dodoma na mikoa jirani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja  na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Bouygues International ya nchini Ufaransa  Eric Fleurisson baada ya kumalizika kwa Mazungumzo,Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. Oktoba 15,2021.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya Bouygues International ya nchini Ufaransa  Eric Fleurisson Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Oktoba 15,2021.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...