Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde ameendelea kuboresha maskani,vituo vya Bajaj na Bodaboda Jijini Dodoma kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya wananchi kupumzika na kupata huduma za usafiri.

Mbunge Mavunde ametembelea leo katika kituo namba 25 cha Nkuhungu-Swai kwa ajili ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi vya kujenga upya kituo hicho kwa thamani ya Tsh 2,000,000 ambacho kitatumika kwa Vijana hao kupumzika na kupakia abiria kwa urahisi zaidi.

“Nitajitahidi kufikia maeneo mengi zaidi ili kujenga maskani na vituo bora vya kupumzikia vijana wa Bodaboda na Bajaj.

Nimeshafanya ujenzi katika maeneo zaidi ya 15 ikihusisha Soko la Mwembeni na Eneo la Chato,na sasa najipanga kuwafungia TV na king’amuzi cha AZAM katika vituo vyote ninavyojenga ili mpate nafasi ya kupata habari mbalimbali pamoja na kuangalia mpira”Alisema Mavunde

Wakitoa shukrani zao kwa niaba ya Vijana hao,Diwani wa Kata ya Nkuhungu Mh. Daud Mkhandi na Katibu wa CCM Kata ya Nkuhungu Bi.Ashura Kimwaga wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuwajali Vijana na kuboresha mazingira yao ya kufanyia kazi na kuahidi kuwa bega kwa bega nao kwa hatua zote ikiwemo kuwasimamia kupata mikopo ya Bajaj na Bodaboda pamoja na kuchangia gharama za ujenzi wa kituo hicho.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...