Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KLABU ya Soka ya Yanga rasmi imekwea kileleni na kuongoza Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC Premier League) msimu wa 2021-22 baada ya ushindi wa bao 2-0 dhidi ya wenyeji katika mchezo huo, KMC FC kwenye dimba la CCM Majimaji mjini Songea.

Yanga SC walipata ushindi huo kwa mabao ya Mshambuliaji Fiston Mayele katika dakika ya 6 na bao la pili lilifungwa na Kiungo Mshambuliaji, Feisal Salim (Feitoto) katika dakika ya 11 ya mchezo huo.

Licha ya KMC kucheza kwa jitihada zote walishindwa kabisa kuona lango la Yanga lililokuwa linalindwa na Golikipa Djigui Diarra akiwa na walinzi wake, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job wakisaidiwa na Kibwana Shomari na Djuma Shamani.

Yanga SC wanaongoza Msimamo wa Ligi hiyo baada ya ushindi wa michezo yote mitatu wakianza na Kagera Sugar FC (1-0) ugenini Bukoba na wakipata ushindi kama huo wa 1-0 dhidi ya Geita Gold FC katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...