NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Katika
kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita Mbunge wa Jimbo la
Kibaha mjini Silvestry Koka amechangia kiasi Cha shilingi milioni 2 kwa
ajili ya mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata ya Sofu
iliyopo katika halmashauri ya mji Kibaha.
Hayo
yamebainishwa na Mbunge hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kata
ya Sofu yenye lengo la kusikiliza kero na changamoto mbali mbali
zinazowakabili wananchi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Koka
katika ziara hiyo ambayo ameambatana na viongozi mbali mbali wa Chama
sambamba na wakuu wa idara na viongozi wa taasisi ametumia fursa ya
ziara hiyo kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo.
"Leo
nipo naendelea na ziara yangu katika kata ya Sofu na nimebahatika
kutembelea baadhi ya miradi yetu ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari n
msingi pamoja na ujenzi wa zahanati ambayo itakuwa na adhi ya kituo Cha
afya,"alisema Koka.
Pia
Koka alibainisha kuwa anatambua Kuna baadhi ya wanafunzi wanakabiliwa na
changamoto ya kutembea umbari mrefu kwa hivyo mradi huu utakuwa ni
mkombozi mkubwa kwa watoto wetu.
Aidha
alisema lengo lake kubwa kwa kushirikiana na serikali ni kuimarisha
zaidi kuboresha miundombinu mbali mbali ya majengo ya wanafunzi pamoja
na madawati ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafika.
Koka
aliongeza katika kata ya Sofu Kuna baadhi ya changamoto mbali mbali
katika sekta tofauti hivyo atahakikisha anasimamia vizuri ili kuweza
kuzitatua changamoto hizo.
Katika
hatua nyingine Koka alibainisha kuwa kwa Sasa Kuna ugonjwa hatari wa
Uviko 19 hivyo wananchi waondokane na hofu na badala yake amewahimiza
kuzingatia maelekezo ya wataalamu ikiwemo kuchoma chanjo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kibaha Mussa Ndomba
alisema kutokana na mchango wa Mbunge hiyo wameamua shule hiyo pindi
itakapokamilika itapewa jina la Koka secondari .
Ndomba
alisema kuwa Koka amekuwa mstari wa mbele katika kuchagiza suala zima
la maendeleo katika sekta mbali mbali hivyo umuhimu wake katika jamii ni
mkubwa Sana.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kushoto
akizungumza Jambo na makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Mussa
Ndomba kuhusiana na mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari inayojengwa
kata ya Sofu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...