Mkuu wa wilaya ya moshi Saidi Mtanda akizungumza katika ibada ya maziko ya aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha kombo kata ya kibosho magharibi aliyeuawa na mwili wake kukutwa umetupwa shambani kwake siku ya jumatano
Mkuu wa kituo cha Polisi Moshi.SSP Pili Misungwi akitoa salamu za pole kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Kijiji cha Kombo Joachim Sakaya.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Said Mtanda , Katikati ni Katibu Tawala Wilaya ya Moshi Angelina Lubella wakimsikiliza mtoto wa marehemu James Sakaya ( Mtoto wa marehemu) .
Na.Vero Ignatus, Kilimanjaro
Jamii imehaswa kujenga utamaduni wa maridhiano ,pale changamoto inapo tokea katika familia au jamii husika ili kuepesha madhara ambayo yanayoweza kutokea ikiwemo kudhuriana ,au kusababisha kifo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Said Mtanda October 09,2021 katika ibada ya maziko ya Joachim Sakaya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji Cha Kombo ,Kata Kibosho Magharibi Wilaya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
"Kila mmoja wetu pana mahali anasali wengine ni KKKT,KATHOLIC,WASABATO, WAISLAM ,lakini tumuogopeni Mungu unamuua binadamu mwenzako unapata faida gani? Ardhi si chochote si lolote tutakufa tutaiacha tuwe na maridhiano " Alisema Mtanda .
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Moshi Pili Msungwi, ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwafichua wale wote wanao chukua sheria mkononi na kusababisha maradhara.
"Kama unazo taarifa za tukio hili, au taarifa zozote zinazo husiana na wahalifu ,wavunja sheria za Nchi na uvunjifu wa amani toeni taarifa hizo kwa Jeshi la Polisi ili kukata mnyororo huo usiendele." Alisema Pili.
James Joachim Sakaya ni Mtoto wa Marehemu amesema Marehemu baba yake alitoka Nyumbani siku ya Jummane kuelekea katika shughuli zake za kiutendaji na hakurudi Nyumbani hadi pale mwili wake ulipo kutwa umetupwa shambani kwake siku ya Jumatano.
Sakaya amesema awali ulikuwepo ugomvi wa kifamilia kati ya ndugu wa Baba Mkubwa na mdogo,hivyo hadi Sasa bado hawajatambua Kama ndio uliopelekea kutokea kwa tukio hilo ama la.
Tukio hili kwetu sisi kimetuumiza.sana mioyo yetu,kwa vile Serikali ipo Basi tumeamua kuwaachia wao watusaidie vya na vifanye kazi yake,hadi Sasa hatujaelewa nini chanzo Cha baba yetu kuuwawa.alisema James
Diwani wa Kata hiyo Kibosho Magharibi Prosper Massawe amesema tukio la mauaji ni la pili kutokea eneo hilo, ambapo mwaka jana 2020 aliuwawa Mwalimu, hivyo wao kama viongozi wa eneo husika kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, wataitisha mkutano wa kulaani vitendo kama hivyo kwani vinaichafua kata hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...