MAHAKAMA Kuu Divisheni  ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa 'Mafisadi' imetupilia mbali Mapingamizi yaliyowekwa na upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi Msingi ya ugaidinm inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu wakipinga kwa kupokelewa kwa maelezo ya onyo ya mshitakiwa wa Adam Kasekwa kwa madai  kuwa yalichukiliwa nje ya muda na na kwamba aliteswa hayana mashiko kisheria 

Kufuatia uamuzi huo Mahakama imeyapokea maelezo ya Kasekwa na kusema ushahidi unaonyesha maelezo hayo yalitolewa na mshatakiwa kasekwa kwa hiyari yake na kwamba yalichukuliwa ndani ya muda.

Uamuzi huo umetolewa leo Oktoba 19,2021 na Jaji Kiongozi, Mustapha Siyani, Hivyo jaji Siyani amejitoa Katika Kesi hiyo  kutokana na Majukumu mengine aliyonayo baada ya Kuteuliwa  Kuwa jaji Kiongozi hivyo atashindwa Kusikiliza Kesi Hiyo kwa mfululizo  kama Inavyotakiwa.

 Hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi pale  ambapo Msajili wa mahakam atampanga Jaji Mwingine wa Kuendelea Na Kesi Hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...