kongamano la wadau wa Pass trust, katika uwezeshaji kilimo biashara leo 6/10/2021 lililofanyika hoteli ya SG Jijini Arusha
Mkui wa mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza katika kongamano la wadau wa Pass trust, katika uwezeshaji kilimo biashara 6/10/2021
Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust Yohane Kaduma, akizungumza katika kongamano la wadau wa Pass trust, katika uwezeshaji kilimo biashara 6/10/2021
Meneja wa( Pass)Kanda ya Kaskazini Hellen Wakuganda akizungumza katika kongamano la wadau wa Pass trust, katika uwezeshaji kilimo biashara leo 6/10/2021
Pichani ni baadhi ywafanyakazi kutoka Taasisi inayojishughulisha na kusaidia sekta ya kilimo Nchini (PASS)
Leah ayoub Meneja Maendeleo ya biashara kutoka PASS akizungumza na wadau katika Kongamano lililofanyika hotel ya SG Jijini Arusha

Na.Vero Ignatus,Arusha
Taasisi inayojishughulisha na kusaidia sekta ya kilimo Nchini (PASS)imeweza kuwawezesha watanzania takriban million 1.7 kupitia udhamini wa miradi 51,627 yenye thamani ya shillingi trillioni 1.22 kwa dhamana ya shillingi billioni 551.4.
Akizungumza katika kongamano la wadau wa Pass trust, katika uwezeshaji kilimo biashara leo 6/10/2021 Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust Yohane Kaduma, amesema kwamba asilimia 47 ya wanufaika hawa ni akina mama,Kupitia udhamini huo PASS na imeweza kutengeneza ajira million 2.6
Kaduma amesema shughuli kubwa ya taasisi hiyo ni kuwezesha wakulima kupata mikopo katika taasisi za fedha, kupitia udhamini wa kati ya asilimia 20-60 kwa wafanya biashara za kilimo ,ambao wanapata changamoto za kukopa kwenye benki kutokana na kukosa dhamana ya kutosha.
"Tunawasaidia wafanyabiashara wa kilimo katika kuandaa mipango ya biashara ambayo inauza ili waweze kupata mikopo katika benki"Alisema Kaduma
Katika mwaka uliopita wa 2020 pekee, takriban miradi 2,375 yenye dhamani ya mikopo ya billioni 12,522,728 ilidhaminiwa na PASS Trust kwa kiasi cha shillingi billioni 6, kuwanufaisha wakulima wa Mkoa wa Arusha pekee.
Aidha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, PASS Trust imedhamini mikopo ya kiasi cha shillingi bilioni 56,623,663,618 tangu mwaka wa 2017 hadi mwaka huu 2021, mikopo ambayo iliwafikia wajasiriamali takriban 3,291 ikijumuisha wakubwa, wa kati na wadogo, katika mkoa huu wa Arusha.
Akifungua kongamano la wadau wa (Pass)Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela alisema amefurahi Kuona miongoni mwa wanaoshiriki vikao hivyo ni pamoja na wadau wa taasisi za fedha, taasisi za kuuuza zana za kilimo, wauzaji wa bidhaa za kilimo , taasisi za serikali , wasafirishaji wa mazao ya kilimo, wavuvi, wafugaji, wakulima miongoni mwa wajasiriamali wengine katika mnyororo mzima wa thamani wa kilimo, uvuvi na ufugaji.
"Sina shaka mkutano huu utasaidia kuchochea maendeleo kwa wananchi na kuchangia katika jitihada za kupunguza umaskini, kwa kuongeza uelewa na kuhamasisha wananchi kuhusu fursa zilizopo katika taasisi ya PASS."Alisema Mongela
Aidha Katika kutekeleza malengo ya Taasisi hiyo , amesema kuwa PASS imeendelea kuzingatia sera ya viwanda kwa kuhakikisha inasaidia sekta ya uzalishaji mazao kwa ajili ya viwanda,pamoja na shughuli nyingine zote zinazounda mnyororo wa thamani wa kilimo.
"Niwapongeze sana PASS Trust kwa juhudi hizi za kuzindua huduma hii ambayo itahakikisha kwamba wale wanaonufaika na udhamini wa PASS Trust, pia wanazingatia utunzaji wa mazingira,Kama mkuu wa Mkoa wa Arusha, nimefurahi kwa kunichagua kuzindua mradi huu, na niseme kwamba,nitaunga mkono juhudi zote za PASS Trust katika utunzaji wa mazingira katika mkoa wangu wa Arusha"
PASS Trust imetimiza miaka 21 tangu kuanzishwa na serikali ya Tanzania pamoja na ile ya Denmark,kwa madhumuni ya kuchochea ukuaji wa kilimobiashara nchini, kupitia upatikanaji wa mitaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...