Na Khadija Kalili, Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge ametoa rai kwa Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Pwani kusimamia ujenzi wa mpangilio wa katika maeneo yote ya vituo vinavyopitiwa na reli ya Kisasa (SGR) alisema hayo leo alipofanya ziara ya kutembelea reli hiyo katika Bandari Kavu iliyopo Kwala.
RC Kunenge alitoa maagizo hayo kwa Wakurugenzi Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Mkoa wa Pwani huku akiwasisitiza kusimamia ujenzi wa kisasa na utakaofuata ramani katika maeneo yote ya eneo hilo liweze kuvutia kwa kuzingatia mipango miji.
Akizungumzia kuhusu hali ya usalama wa miradi hiyo mikubwa na ya kimkakati ambayo ni SGR na Bwawa la Mwalimu Nyerere lililopo Rufiji alisema kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama tayari wamesha wabaini wahujumu wa miundo mbinu hiyo na tayari wamefikishwa Mahakamani na ana imani kubwa watachukuliws hatua kali za kisheria Ili wawe mfano.
"Wiki iliyopita Makamu wa Rais Dkt. Philip Isidory Mpango alifanya ziara ya siku mbili Mkoani hapa ambapo alionyesha kusikitishwa kwake na wahalifu wa miundombinu ya miradi yetu ya SGR na Bwawa la Mwalimu Nyerere huku akiahidi kuwa serikali haitowavumulia wahujumu hao na kumtaka RC , Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Pwani kuwashughulikia na sisi tunetimiza" alisema RC Kunenge.
Alisema kuwa hivi sasa miradi hiyo inasimamiwa kwa nguvu imara zaidi na ameahidi kutokuwa na mianya ya hujuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...