* RAS Wote Simamieni Utekelezaji wa Anwani za Makazi kwenye Maeneo Yenu
 
Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anakuwa na anwani za makazi ifikapo mwaka 2022.
 
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.  Zainab Chaula katika semina ya kujenga uelewa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanzania Bara kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi.
 
"Tunatarajia kufikisha mawasiliano mpaka vijijini, tunataka nchi nzima iwe na anwani ya makazi," amedokeza Dkt. Chaula.
 
Aidha, amehabarisha kuwa baadhi ya faida za kuwa anwani za makazi ni kurahisisha ukusanyaji kodi, kuwezesha biashara mtandao na kuimarisha ulinzi na usalama.
 
Awali, akifungua semina hiyo, Katibu Mkuu wa  Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof. Riziki Shemdoe amesema Serikali za Mikoa zina majukumu ya kusimamia utekelezaji wa anwani za Makazi kwenye maeneo yao 
 
"Serikali yetu ya Tanzania kupitia Sera ya Posta ya mwaka 2003 imeimarisha mifumo ya anwani za makazi inayoundwa na barabara, njia na namba za nyumba," amebainisha.
 
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo amesisitiza ushirikiano ili kufikia malengo kwa kuwa moja ya manufaa ya anwani hizo ni kuwezesha na kufanikisha utambuzi wa majengo na viwanja vilivyopo ili kurahisisha kazi ya mipango miji na utekelezaji wa majukumu ya kiuchumi na kijamii kwa Serikali na wananchi kwa ujumla
 
"Naamini tutaendelea kushirikiana katika kujenga nchi yetu na kuwahudumia Watanzania," ametanabaisha Bi. Makondo
 
Ibara ya 61(m) ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 inaielekeza Serikali iliyopo madarakani kuhakikisha anuani za makazi zinawekwa nchini ili kurahisisha upatikanaji, utoaji na ufikishishaji wa huduma mbali mbali kwa wananchi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akizungumza kuhusu aina mbalimbali za vibao vya anwani za makazi wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi iliyofanyika Oktoba 21, 2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akizungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara katika semina ya kuwajengea uelewa kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi iliyofanyika Oktoba 21, 2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula (kulia) akiteta na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi iliyofanyika Oktoba 21, 2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe  akizungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, katika semina ya kuwajengea uelewa kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi iliyofanyika Oktoba 21, 2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo akizungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara katika semina ya kuwajengea uelewa kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi iliyofanyika Oktoba 21, 2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakisikiliza kwa umakini maoni ya Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara katika semina ya kuwajengea uelewa kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi iliyofanyika Oktoba 21, 2021 jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, waliokaa mbele kulia wakifuatilia makala maalumu kuhusu umuhimu na matumizi ya anwani za makazi wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi iliyofanyika Oktoba 21, 2021 jijini Dodoma.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa anwani za makazi katika jiji la Mwanza ambayo ni Halmashauri ya mfano wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi iliyofanyika Oktoba 21, 2021 jijini Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Prof. Faustine Kamuzora akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi iliyofanyika Oktoba 21, 2021 jijini Dodoma.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...