Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (aliyevaa Miwani) wakati alipotembelea mtaa wa Hesawa jijini Mwanza kujionea uwekaji wa anuani za makazi katika nyumba mbalimbali pamoja na usimikaji wa nguzo zenye vibao vya majina katika mitaa 175 ya jiji hilo.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel akimwelezea Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji (wa kwanza kulia) namna Jiji la Mwanza linavyotekeleza uwekaji wa anuani za makazi na usimikaji wa nguzo zenye vibao vya majina ya mitaa katika mitaa 175 ya jiji hilo, wakati alipotembelea mtaa wa Hesawa jijini Mwanza kujionea uwekaji wa anuani hizo.

Diwani wa Kata ya Nyamagana Jijini Mwanza Mhe. Biko Kotecha akizungumza kwa niaba ya wakazi wa Mtaa wa Hesawa Jijini Mwanza wakati wa ziara ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji (wa kwanza kulia) Jijini humo kujionea utekelezaji wa anuani za makazi wakati alipotembelea mtaa huo.Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Robert Gabriel.


Mwonekano wa nyumba zilizowekewa namba za nyumba katika jiji la Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa anuani za makazi katika jiji hilo ambapo jumla ya nyumba 108, 000 tayari zimewekwa namba kwenye mitaa 175.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...