Na Mwandishi Wetu, Arusha

SHIRIKA la Posta Mkoa wa Arusha limepanga kutembelea na kutoa misaada kwa watoto wenye uhitaji katika Gereza Kuu la Kisongo,mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 6,2021 ofisini kwake,Meneja wa Shirika hilo mkoani hapa, Athman Msilikale amesema wanatarajia kutoa misaada hiyo Oktoba 9, mwaka huu wakati wa maadhimisho ya siku ya Posta duniani.

Amesema maadhimisho haya ambayo kitaifa yatafanyika jijini Dodoma,yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu kwa Posta Endelevu”.

Amesema kutokana na shirika hilo kuwa la serikali hivyo linashirikiana na wananchi na kuwa mkoani hapa wameona kwa kuwa wanapaswa kurejesha faida kwa jamii,kutumia maadhimisho hayo kukutana na kundi hilo la watoto ambao wanaishi katika mazingira hayo.

“Lengo ni kuwafariji ili wasijione wametengwa na jamii,hasa baada ya wengine wazazi wao kuhukumiwa,tunapaswa kutambua kuwa wana mahitaji hivyo tunatatoa misaada kulingana na mahitaji yao,”amesema meneja huyo.

“Hili ni shirika la serikali,tunaona ni muhimu tuipeleke kwa wananchi kwa sababu tunaona ni vizuri tukashirikiana na wananchi kwa pamoja,”amesema.

Kuhusu elimu kwa jamii amesema watatumia fursa hiyo kuelezea huduma zao za posta ambazo wamekuwa wakizifanya ikiwemo utumaji wa barua,nyaraka na vifurushi kupitia huduma ya EMS.

Ameeleza shirika hilo la Kimatiafa lina mtandao mkubwa kuanzia kidunia, Afrika tuna kuliko mashirika mengine ambapo duniani kuna vituo vya kutoa huduma zaidi ya 600,000.

 

Meneja wa Shirika la Posta,mkoa wa Arusha,Athman Msilikale akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya Siku ya Posta duniani,yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 9,2021(Picha na Mpigapicha Wetu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...