Charles James, Michuzi TV

MKURUGENZI Mkazi wa Shirika la Christian Blind Mission Tanzania (CBM) Bi Nesia Mahenge,amewataka wadau mbalimbali kuhudhuria maonyesho ya wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) ambayo inatarajiwa kuanza kesho ili kujionea mchango wa AZAKI  katika maendeleo ya Taifa.

Hayo ameyasema leo Oktoba 22,2021 wakati akizungumza na waandisi wa habari kuhusu wiki ya AZAKI ambayo inatarajia  kuanza kesho Oktoba 23,2021 jijini Dodoma na kufunguliwa na Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai.

Mahenge amesema kuwa  jumla ya Asasi zaidi ya 150 zitashiriki katika maonyesho hayo  lengo likiwa ni kuonyesha mchango wake katika maendeleo ya Taifa. 

Aidha amesema kuwa wiki hiyo inawaleta wadau mbalimbali wa Maendeleo nchini ikiwemo Wananchi,Serikali,AZAKI na sekta binafsi  kwa pamoja ili kujadili na kusherehekea mchango wa AZAKI katika kuleta maendeleo nchini.

"Tunawaita  wadau mbalimbali wa maendeleo kujumuika nasi kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo   ushauri wa kisheria,kufahamu kazi tunazofanya na kusherehekea kwa pamoja ,"amesema Mahenge

Amesema kuwa katika uzinduzi  wa wiki ya AZAKI utahudhuriwa na wahisani wa maendeleo wakiwemo ubalozi wa Denmark Utakaowakilishwa na Sascha Mulla na Ubalozi wa Canada útawakikishwa na Ms.Helen Fytche.

Hata hivyo Mahenge amesema kuwa  Asasi za kiraia zipo katika mchakato wa kufanya  utafiti  ni mchango kiasi gani  wameutoa katika shughuli mbalimbali.

Amesema wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za  kuleta maendeleo  kwa kushirkiana na Serikali  na kwamba wamepewa   miongozo mbalimbali na Serikali katika kuingia  ubia wa  kuleta maendeleo.

Amesema wanafanya shughuli mbalimbali katika  sekta za  elimu,kilimo,afya na masuala ya ajira, kuwajengea uwezo na maeneo mengine  mengi.

“Na kuna tafiti  tunataka kuufanya na  tumeishaanza mchakato kuweza kuangalia kwa takwimu maalum ni michango ya kiasi gani kama ni rasilimali fedha,watu,vifaa mbalimbali ambavyo vinatolewa  na huduma ambazo zinatolewa  kuweza kujua tumefanya kwa kiasi gani.

“Nadhani huo utafiti utasaidia sana kutoa picha kamili kuweza  kuonesha mchango ambao tunatoa katika Nchi ya Tanzania,”amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa United Nations Association (UNA) Reynald Maeda amewataja Viongozi na wageni mbalimbali kutoka Serikalini watakaoshiriki katika uzinduzi huo ni pmaoja na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,Meya wa Jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe na mwakili kutoka Wizara ya Afya Vickness Mayao.

"Katika kusherehekea mafanikio  ya sekta ya AZAKI na ubia Wetu baina ya wananchi maonyesho yatakayofanyika tarehe 23 hadi 24 Oktoba Katika ukumbi wa Jakaya Kikwete na kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Profesa Jay,Sheta,Barnabas,Gnako,na wasanii wa Dodoma,"amesema.

Amesema  kuwa wiki ya AZAKI hukutanisha wadau wa maendeleo kujadili masuala ya masingi kuhusu ustawi wa sekta pamoja na maendeleo ya Taifa Kwa ujumla



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...